Loading...

Real Madrid yataja bei ya Gareth Bale


Gareth Bale aliiteka dunia kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kufunga magoli mawili, ikiwa ni pamoja na moja lakuvutia ambalo lilikuwa la kwanza wakati alipofunga goli la kwanza la kushangaza.

Lakini maoni ya hivi karibuni baada ya mchezo huo yamekuwa yakimhusisha na kuachana na vigogo hao wa Uhispania.

Taarifa ya Daily Star inadai kwamba Real Madrid wamepanga kiasi kibubwa cha fedha kati ya pauni milioni 200 na 230 kuwa ada ya uhamisho wa Gareth Bale.

Gareth Bale alisema kuwa atafanya mazungumzo zaidi na wakala wake kwenye majira ya joto kuhusu hatima yake katika klabu ya Real Madrid, huku Manchester United, Chelsea, Bayern Munich na klabu yake ya zamani, Tottenham zikihusishwa na raia huyo wa Wales.
Real Madrid yataja bei ya Gareth Bale Real Madrid yataja bei ya Gareth Bale Reviewed by Zero Degree on 5/28/2018 11:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.