Loading...

UEFA watangaza mshindi kimakosa wiki 2 kabla ya fainali kuchezwa

Fainali itachezwa mjini Kiev, tarehe 26 Mei
UEFA walitangaza mshindi wa Ligi ya Mabingwa msimu huu kuwa Liverpool kwenye tovuti yao mapema siku ya Ijumaa.
Kwa mujibu wa taarifa ya 'Mirror', maneno yaliyoashiria kuwa Liverpool ni mshindi wa taji la Ligi ya Mabingwa msimu wa 2017/18 yalionekana kwenye ukurasa mmoja wa michuano hiyo.

Liverpool watamejwa kuwa washindi wa Ligi ya Mabingwa kwenye tovuti ya UEFA
Chini ya beji ya Liverpool liliwekwa neno Mshindi (Winner). Liverpool itakabiliana na Real Madrid kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa mjini Kiev, tarehe 26 Mei.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kosa hili lilirekebishwa haraka lakini baada ya kuwa watumiaji wa mtandao wa twitter wameshagulindua hilo na kuliweka kwenye mtandao huo wa kijamii.

Fainali itachezwa mjini Kiev, tarehe 26 Mei
UEFA watangaza mshindi kimakosa wiki 2 kabla ya fainali kuchezwa UEFA watangaza mshindi kimakosa wiki 2 kabla ya fainali kuchezwa Reviewed by Zero Degree on 5/04/2018 09:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.