Loading...

UEFA yatangaza sheria mpya zitakazotumika kuanzia msimu ujao


Timu zitakazoshiriki UEFA msimu ujao zitaruhusiwa kufanya 'sub' ya mchezaji wa nne kwenye muda wa nyongeza (Extra Time) na kutumia wachezaji wapya waliosajiliwa kutoka vilabu vingine hata kama wameshashiriki michuano hiyo katika klabu zao za awali.

Mabadiliko haya ni miongoni mwa mabadiliko kadhaa yaliyofanywa na Bodi ya mpira wa miguu barani Ulaya leo Jumanne na yanafuata maamuzi ya Kamati Tendaji ya UEFA mwezi Februari na ya Chombo cha Sheria za Michezo pamoja na Bodi ya Shirikisho la Soka Kimataifa, mapema mwezi huu.

Kuanzia msimu ujao, klabu zitazocheza Super Cup na kufika fainali za Ligi ya Mabingwa na Ligi ya Europa zitaruhusiwa kuwa na wachezaji 12 wa akiba 'sub' katika benchi, ambapo kwa kawaida benchi linatakiwa kuwa na wachezaji 7.

Katika tamko, UEFA ilisema "Makocha wana wigo mpana wa kufanya mabadiliko ya wachezaji, na kuweza kuwa na usimamizi mzuri wa vikosi vyao kwenye mechi muhimu ndani ya msimu husika".

Suala la kuwepo kwa 'sub' ya mchezaji wa nne kwenye muda wa nyongeza limeshafanyiwa majaribio katika moja ya michuano ya UEFA na inaruhiswa kwenye michuano ya FA Cup msimu huu.

Hata hivyo, Uamuzi wa kuruhusu vilabu kusajili wachezaji wapya watatu "bila kuwa na kizuizi chochote" baada ya hatua ya makundi, unaweza kuleta utata, kwani linaondoa ile kanuni ya kumzuia mchezaji kuichezea klabu mpya kama atakuwa ameshashiriki michuano hiyo akiwa na klabu yake ya awali. Kwa mfano, kama sheria hiyo ingekuwepo msimu huu, Philippe Coutinho angekuwa na uwezo wa kuichezea Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa, licha ya kwamba ameshaichezea Liverpool tayari.

Lakini UEFA ina amini kuwa inajaribu kuleta sheria zake ziendana na sheria za ligi za ndani barani Ulaya.
UEFA yatangaza sheria mpya zitakazotumika kuanzia msimu ujao UEFA yatangaza sheria mpya zitakazotumika kuanzia msimu ujao Reviewed by Zero Degree on 3/27/2018 11:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.