Loading...

Abdul Nondo asimamishwa masomo UDSM


Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimemsimamisha kuendelea na masomo mwanafunzi wake wa mwaka wa tatu, Abdul Nondo baada ya kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa.

Nondo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), amesimamishwa masomo kuanzia Machi 26, 2018 kwa barua iliyoandikwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye.

Kwa mujibu wa taarifa ya Gazeti la Mwananchi, Profesa Anangisye amesema, “ni kweli barua ya kumsimamisha ni yangu na tumefanya hivyo kwa mujibu wa tararibu zetu.”
Abdul Nondo asimamishwa masomo UDSM Abdul Nondo asimamishwa masomo UDSM Reviewed by Zero Degree on 3/27/2018 11:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.