Loading...

Viongozi Chadema wawekwa mahabusu Sentro


Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe Freeman Mbowe na baadhi ya viongozi wengine waandamizi wa chama hicho akiwepo Katibu Mkuu Dkt Vincent Mashinji, John Mnyika, Salum Mwalimu na Ester Matiko wamewekwa mahabusu.

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha hilo na kusema kuwa viongozi hao wamewekwa mahabusu baada ya kuripoti Kituo Kikuu Cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao.

"Viongozi Wakuu wa Chama pamoja na wabunge waliokuwa wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao, wamewekwa mahabusu. Polisi hawajaeleza sababu ya kufanya hivyo. Mawakili wetu wanashughulikia. Tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi" alisema Makene 

Aidha Makene amesema kuwa viongozi hao wamefutiwa dhamana yao kwa maelekezo ya Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZCO) pia jeshi la polisi limedai viongozi hao watafikishwa mahakamani Jumatano, Machi 28, mwaka huu.
Viongozi Chadema wawekwa mahabusu Sentro Viongozi Chadema wawekwa mahabusu Sentro Reviewed by Zero Degree on 3/27/2018 12:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.