Loading...

Vigogo Ligue 1 wanaongoza mbio za kuwania saini ya nyota wa Chelsea


Vigogo wa Ligi Kuu ya Ufaransa, AS Monaco wanaripotiwa kuwa tayari kumpa David Luiz ofa ya kuondokana na adha ya kupigwa benchi katika klabu ya Chelsea kwenye majira ya joto.

Mbrazil huyo alipata nafasi ya kuanza na kikosi cha kwanza kwenye mechi 9 pekee za Ligi Kuu ya Uingereza chini ya Antonio Conte msimu huu na anaonekana ana mpango wa kuondoka Stamford Bridge kama meneja wake ataendele na kibarua chake.


Alitoka kwenye hatua ya kuwa beki bora wa katikati kwenye ligi hadi kuwa mmoja wa waliosahaulika.

David Luiz
Baada ya kutofautiana na meneja wake kufuatia Chelsea kufungwa na AS Roma mapema msimu huu kulimuacha Luiz kwenye wakati wakuwa kama mtazamaji wa nje – mchezo wake wa mwisho kuanza na kikosi cha kwanza ilikuwa ni dhidi ya Watford mwezi Februari.

Kwa mujibu wa ripoti za usajili za Uingereza, mabingwa hao wa mwaka jana Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1), Monaco wangekuwa na furaha kumsajili beki huyo mwenye umri wa miaka 31 kutoka London, ikiwa ni katika harakati za kerejesha ubingwa wa Ligue 1.
Vigogo Ligue 1 wanaongoza mbio za kuwania saini ya nyota wa Chelsea Vigogo Ligue 1 wanaongoza mbio za kuwania saini ya nyota wa Chelsea Reviewed by Zero Degree on 5/02/2018 01:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.