Loading...

Odinga awataka wafuasi wake waache kususia bidhaa za kampuni nne Kenya

Odinga awataka wafuasi waache kususia bidhaa za kampuni nne Kenya
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amewaambia wafuasi wake wasitishe kampeni ya kususia bidhaa na biashara za kampuni zilizohusishwa kuwa na uhusiano na chama tawala nchini Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta.
Safaricom, kampuni kubwa ya mawasiliano ya simu nchini na Brookside, ambayo ni kampuni ya kutengeneza bidhaa kama maziwa na siagi nimiongoni mwa kampuni zilizolengwa.

Bwana Odinga alitoa tamko hilo leo katika sikuukuu ya Mei mosi au 'Leba dei' katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.

'Tulikuwa na hasira nyingi kwa yale makampuni yaliokuwa yanaunga mkono serikali ya Jubilee. Tukasema safaricom, Brookside, Bidco na tukaongeza Haco, tulisema ni makampuni ambayo yanatesa watu wetu, ambayo yamekataa kukubali uamuzi wa wananchi na tukasema watu wetu wote wasusie bidhaa za kampuni hizo.
'Sasa tumeshikana mkono na Uhuru, tumekubaliana kufanya kazi pamoja tusulishe mambo, na tumeweka sasa kamati ya ushauri ya kuleta suluhu ya kudumu. Kwa hiyo leo hii tunatangaza tunatoa ile amri ya kususia'. Alitangaza Raila Odinga mbele ya umati wa watu waliokusanyika katika bustani ya Uhuru mjini Nairobi kwa sherehe hizo za Mei Mosi.

Kampuni ambazo Nasa ilisema wafuasi wake izisusie ni:

  • Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom, ambayo ndiyo tajiri zaidi miongoni mwa kampuni za Kenya
  • Kampuni ya maziwa ya Brookside, inayomilikiwa na familia ya Kenyatta
  • Kampuni ya kutengeneza mafuta ya kupikia na sabuni ya Bidco
  • Kampuni ya Haco inatengeneza na kusambaza bidhaa za urembo, na za usafi wa nyumba nchini Kenya, Uganda, na Tanzania

Muungano wa upinzani Nasa uliyaorodhesha makampuni hayo kwa kile ilichokitaja kuunga mkono utawala usio halali uliomnyima Raila ushindi katika uchaguzi mkuu mwaka jana.

Mnamo mwezi Machi mwaka huu kiongozi huyo mkongwe wa kisiasa Kenya alipatana na rais Uhuru Kenyatta na viongozi hao wawili kwa sasa wanashirkiana katika 'kujenga madaraja'.
Tangazo hilo la kususia bidhaa za wanaotajwa kuwa washirika wa chama tawala lilitolewa mnamo Novemba mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na mzozo ulioshuhudia Kenya kuwa nchi ya kwanza Afrika na ye nne pekee duniani kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais.

Raila Odinga amesema maafikiano yake na Uhuru Kenyatta yalioidhinishwa kwa kusalimiana kwa mikono viongozi hao wawili mnamo Machi 9, yamechangia amani na kuruhusu Wakenya kuendelea.

Tangazo la leo litaonekana kama mfano mwingine wa kupatana na kurudi kwa uhusiano mwema baina ya viongozi wawili.
Odinga awataka wafuasi wake waache kususia bidhaa za kampuni nne Kenya Odinga awataka wafuasi wake waache kususia bidhaa za kampuni nne Kenya Reviewed by Zero Degree on 5/02/2018 01:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.