Loading...

Burundi kuitambulisha katiba mpya siku ya Alhamisi

Rais Pierre Nkurunziza akipiga kura ya mapendekezo ya katiba
Hata hivyo wapinzani na baadhi ya nchi za kigeni wamekosoa mchakato huo mzima kwamba haukuzingatia sheria na katiba mpya inanuwia kumbakiza madarakani Rais Pierre Nkurunziza hadi mwaka 2034.

Taarifa ya Ikulu ya Burundi imethibitisha kuwa sherehe za utiaji sahihi kwenye katiba mpya na kuitambulisha kwa raia zitafanyika alhamisi saba katika mkoa wa kati wa Gitega eneo la Bugendana ambako huko ndiko kulikozinduliwa rasmi mchakato wa katiba, lakini pia kampeni ya chama madarakani CN DD/FDD ya kuipiga debe katiba hiyo.

Aidhaa taarifa hiyo ya Ikulu imetoa mwaliko kwa magavana wote na Wakuu wa tarafa za Burundi kushiriki kwenye sherehe hizo. Wamealikwa pia wawakilishi wa vyama vya kisiasa , asasi za kiraia pamoja na Viongozi wa kidini .

Itakuwa mara ya kwanza katika historia ya Burundi kuwa na sherehe za kuipokea katiba mpya. Wadadisi wa siasa za Burundi wanahisi utaratibu huo mpya ni ujumbe wa Rais Nkurunziza wa azama yake ya kukamilisha shughuli ya katiba ambayo yeye ameipigia debe kwamba inakuja kuipa Burundi hadhi na Uhuru wake kamili wa kujitawala .

Lakini pia ni ujumbe ambao kiongozi huyo anaupeleka kwa Jumuiya ya kimataifa hususan, mataifa ambayo yalitilia shaka na kukosoa mpango mzima wa marekebisho ya katiba wakitaja kwamba uliandaliwa kinyume cha sheria .

Ni hivi majuzi tu Umoja wa mataifa, na baadhi ya nchi za magharibi washirika wa zamani wa Burundi kama Ufaransa na Ubelgiji walikemea vikali mchakato mzima wa katiba kwamba uligubiikwa na dosari nyingi na kwamba katiba hiyo mpya inatishia hata maridhiano ya kitaifa na uwakilishi wa makabila kwa Mujibu wa Mkataba wa Aman iwa Arusha. Madai ambayo yamepingwa vikali na Wakuu wa Burundi.

Katiba hii mpya ambayo inaanza kutekelezwa siku ya Alhamis itageuza mambo mengi kwenye taasisi za maongozi ya taifa , lakini pia kutoa fursa kwa Rais Pierre Nkurunziza kuweza kuwania uongozi wa nchi hadi mwaka wa 2034.

Katiba pia inaanza kutekelezwa wakati mazungumzo ya amani yakiwa yamekwama baada ya serikali kukata kuketi meza moja na wapinzani. Kufuatia hali hiyo ya mkwamo,

Wajumbe wa Muungano wa Ulaya wamelichagiza Shirika la Muungano wa Afrikan kuchukua mikononi mazungumzo ya amani ya Burundi kwa madai kwamba Jumuiya ya kimataifa imeanza kupoteza imani kwa mchakato wa upatanishi unaosimamiwa na Jumuiya ya Afrika ya mashjariki na inayoongozwa na Rais Museveni pamoja na msuluhishi Benjamin Mkapa.

Source: BBC
Burundi kuitambulisha katiba mpya siku ya Alhamisi Burundi kuitambulisha katiba mpya siku ya Alhamisi Reviewed by Zero Degree on 6/05/2018 07:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.