Loading...

Klabu 3 za Ligi Kuu ya Uingereza kushindania saini ya nyota wa Barcelona


Klabu tatu za Ligi Kuu ya Uingereza, Arsenal, Liverpool na Chelsea wana nia ya kumsajili nyota wa Barcelona.

Klabu hizo zinatarajiwa kushindania saini ya golikipa wa klabu ya Barcelona, Jasper Cillessen.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za nchini Uhisapnia – Liverpool, Arsenal na Chelsea zimeifikia Barcelona kuuliza uwezekano wa kumsajili Jasper Cillessen kwenye majira haya ya joto.

Ripoti ya Express inaeleza kwamba mahasimu wa London, Arsenal na Chelsea wamepiga hatua zaidi kwenye mbio hizo za kuwania saini ya mlinda mlango huyo raia wa Uholanzi.

The Gunners wako sokoni kusaka mrithi wa kudumu wa Petr Cech, ambaye alifikisha umri wa miaka 36 mwezi uliopita.

Jasper Cillessen
Wakati huo huo, Chelsea wameulizia kuhusu uwezekano wa kuipata saini ya Cillessen kutokana na mashaka juu ya hatima ya Thibaut Courtois.

Courtois anahusishwa na uhamisho kwenda Real Madrid na mkataba wake unaisha msimu ujao.

Unai Emery anaweza kupendelea kusajili golikipa mpya kwenye majira haya ya joto na Arsenal wamejitokeza kwa kuwasiliana moja kwa moja na Barcelona kufanya majadiliano juu ya uwezekano wa uhamisho huo.

Kwa upande mwingine, Liverpool bila mashaka yoyote watatumia kiasi kikubwa cha fedha kusaka golikipa mpya baada ya makosa yaliyofanywa na Loris Karius kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Wekundu hao pia wamekuwa wakihisishwa na magolikipa wengi.
Klabu 3 za Ligi Kuu ya Uingereza kushindania saini ya nyota wa Barcelona Klabu 3 za Ligi Kuu ya Uingereza kushindania saini ya nyota wa Barcelona Reviewed by Zero Degree on 6/07/2018 08:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.