Loading...

Rivaldo aunga mkono uhamisho wa Fred kwenda Manchester United

Fred aliungana na Neymar kwenye kikosi cha Brazil Kombe la Dunia 2018
Rivaldo anasema Manchester United wanapata ''mchezaji wa uhakika'' baa ya kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa timu ya taifa ya Brazil, Fred.
Fred aliingia kama mbadala kwenye mechi ya kiraafiki iliyomalizika kwa Brazil kushinda mabao 2-0 dhidi ya Croatia katika dimba la Anfield siku ya Jumapili na anatarajiwa kutua Old Trafford kwa mkataba ulioripotiwa kuwa wa miaka mitano.

United walifichua taarifa hiyo kwa ufupi kwenye kauli yao katika tovuti yao, na kuahidi kutoa taarifa zaidi baadae.
Fred amecheza mechi nane tu akiwa na Brazil lakini nisehemu ya kikosi cha wachezaji 23 watakaoliwakilisha taifa hilo kwenye Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, na mshindi wa Kombe la Dunia mwaka 2002, Rivaldo anaamini kiungo huyo ataifaa sana United.

Rivaldo
Kwa mujibu wa taarifa ya Sky Sports, Rivaldo alisema: "Ni mchezaji wa aina yake."

"Kama mchezaji yeyote mwingine wakati unapohamia kwenye nchi mpya, atahitaji muda kidogo kuweza kuendana na makazi mapya.
"Lakini unapokuwa mchezaji mzuri na kiungo mwenye kipaji kama chake, anaenda kufanya vizuri na atakuwa mzuri kwa Manchester United na watakuwa wazuri kwake."

Fred alijiunga na Donetsk mwaka 2013 na alikuwa sehemu ya washindi mara tatu wa Ligi Kuu ya Ukraine.
Aliikabili United kwenye Ligi ya Mabingwa katika dimba la Old Trafford kipindi klabu hiyo inanolewa na David Moyes, na pia alicheza dhidi ya Manchester City kwenye michuano hiyo msimu uliopita Shakhtar ilipofika kwenye hatua ya 16 bora.

Rivaldo aunga mkono uhamisho wa Fred kwenda Manchester United Rivaldo aunga mkono uhamisho wa Fred kwenda Manchester United Reviewed by Zero Degree on 6/07/2018 08:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.