Loading...

Mambo 5 unayotakiwa kujua kuhusu kiungo anayewindwa na Man United, Fred

Fred
Wakati Manchester United ikiendelea kusaka saini ya Fred, hapa chini kuna mambo matano unayotakiwa kujua kuhusu kiungo huyo wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Shakhtar Donetsk mwenye umri wa miaka 25:

1. Alifunga goli lake la kwanza dhidi ya shujaa wake Ronaldinho

Fred ni kiungo mkabaji siku hizi, lakini alianza kucheza kama beki wa kushoto katika klabu ya Atletico Mineiro katika mji anotokea, Belo Horizonte. Alipohamia 
Internacional Porto Allegre katika umri wa miaka 16 mwaka 2009, alitumiwa kama kiungo mchezeshaji katika Academy, na bila ya kushangaza Ronaldinho alikuwa ndiye mchezaji anayemvutia.

Wakati ambapo wakala wa Fred alikuwa Roberto de Assis Moreira, kaka yake na Ronaldinho. Na Fred alifanikiwa kufunga goli lake la kwanza nchini Brazil kwenye michuano ya Kikombe mwezi Julai, 2012 dhidi ya timu yake pendwa ya Atletico Mineiro, ambayo ilimchezesha Ronaldinho. Internacional ilipoteza mchezo huo kwa kuchapwa mabao 3-1 na kocha wao akatimuliwa.

2. Dunga alikuwa na msaada mkubwa kwake

Tabia ya kubadili makocha mara kwa mara katika klabu ya Internacional ilikuwa na faida kubwa kwa Fred na Dunga alimfundisha mambo mengi baada ya kutua mwezi Disemba, 2012. Kwa wakati ule, chipukizi huyo alikuwa anacheza kama kiungo mkabaji na hivyo alikuwa na mtu anayefaa kumpa uzoefu, ambaye ndiye alikuwa nahodha
 wakati Brazil inabeba ubingwa kwenye Kombe la Dunia mwaka 1994.

Dunga alimweka Fred kwenye kundi la wachezaji wake wa muhimu na, wakati alipopata nafasi ya kuinoa timu ya taifa ya Brazil, alimuita kushirikiana naye. Kiungo huyo alijumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kwenye michuano ya Copa America 2015 na alianza na kikosi cha kwanza kwenye michezo miwili pembeni ya Neymar, Roberto Firmino na Fernandinho.

3. Shakhtar walimsajili achukue nafasi ya Fernandinho

Kwenye majira ya joto mwaka 2013, Fred alichaguliwa na mkufunzi wa Shakhtar Donetsk, Mircea Lucescu na Mkurugenzi mtendaji wa klabu, Sergey Palkin arithi mikoba ya Fernandinho, ambaye aliuzwa kwenda Manchester City kwa pauni milioni 34. Internacional walipokea ofa ya pauni milioni 13.14 kwa ajili ya nyota huyo aliyekuwa na umri wa miaka 21 kipindi hicho, ambaye alikuwa Mbrazil wa mwisho kujiunga na klabu ya Ukraine.

Katika hatua nyingine, ilionekana kama vile Fred angefuata nyayo za Mbrazil mwenzake Fernandinho lakini Shakhtar walikataa kufanya makubaliano Man City mwezi Januari, wakidai wanamhitaji mchezaji huyo kwenye hatua ya mtoano kwenye Ligi ya Mabingwa. Fred alikuwa kwenye hatua ya makundi na uamuzi wa kumbakisha ulithibitisha umuhimu wake wakati kiungo huyo alipofunga goli 'free kick' - goli lake la kwanza kwenye michuano hiyo katika mchezo uliomalizika kwa Shakhtar kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Roma katika hatua ya 16 bora.

Sasa inaonekana kama vile Fred anaweza kujiunga na upande mwingine wa  Manchester na kukabiliana na Fernandinho kwenye mechi ya mahasimu wa jiji moja. Haitakuwa mara ya kwanza kwake, baada kuwa amecheza dhidi yake kwenye 
Ligi ya Mabingwa katika hatua ya makundi ya msimu huu.
Fred
4. Paulo Fonseca alibadilisha maisha yake

Imebaki kuana kama kujiunga na Jose Mourinho litakuwa wazo zuri kwake, lakini kocha huyo wa Kireno, 
Paulo Fonseca alisaidia kwa kiwango kikubwa sana kubadilsha maisha ya Fred. Lucescu hakumtumia Fred mara kwa mara lakini, baada ya mchezaji huyo kuondolewa kwenye michuano ya Copa Amerika mwaka 2015 baada kugunduka ametumia dawa za kupunguza msukumo wa damu, alibadilika na kuwa mchezaji wa kuigwa hadi alipofika Paulo Fonseca.

"Fonseca ananiruhusu kucheza kiuadui na kukaba zaidi na jukumu langu kubwa ni kubadilisha mwelekeo wa mashambulizi. Chini ya uongozi wa Lucescu, washambuliaji na mabeki wa pembeni walikuwa na jukumu hilo, lakini kwa sasa mimi ndio muhusika. Kila kitu kilibadilika. Kocha ananiamini na anaona uwezo nilionao, ambao Lucescu hakuuona," alisema.

Fonseca mara kwa mara alitumia mfumo wa 4-2-3-1 ambao Mourinho anapenda kutumia na Fred alinga'ara. Akiwa na uwezo wa kutumia miguu yake yote na uwezo wa kumiliki mpira, aliisaidia Shakhtar kutetea ubingwa msimu huu.

5. Ameitwa kwenye kikosi cha Brazil kwenye Kombe la Dunia 2018

Uhodari kama huo unaweza kuwa ndio umemvutia Tite kufanya uamuzi wenye utata kumjumuisha Fred kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil cha kombe la dunia. Hakupata nafasi ya kucheza kwenye mechi yoyote ya kufuzu kushiriki michuano hii na wachezaji wenye ubunifu kama nyota wa klabu ya Lazio, Felipe Anderson, Talisca wa 
Besiktas na Giuliano wa Fenerbahce walichwa nyumbani kutoa nafasi kwa wachezaji wengine.

Kupata uzoefu katika ngazi za juu inawezakuwa na faida kwake kuelekea uhamisho wake kwenda Old Trafford. Ligi ya Ukraine imeshuka kwa kiasi kikubwa na Fred amefanikiwa kucheza mechi za muhimu. Hilo halitakuwa tatizo kwake.

Source: ESPN
Mambo 5 unayotakiwa kujua kuhusu kiungo anayewindwa na Man United, Fred Mambo 5 unayotakiwa kujua kuhusu kiungo anayewindwa na Man United, Fred Reviewed by Zero Degree on 5/25/2018 09:56:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.