Loading...

Sadio Mane ametuma jezi 300 za Liverpool kijijini kwao

Sadio Mane ametuma jezi 300 za Liverpool kwa mashabiki wa klabu hiyo kijijini kwao
Mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane alituma jezi 300 za klabu yake kwa mashabiki wa katika kijiji cha nyumbani kwao, Bambali nchini Senegal kuelekea fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid.

Familia ya Mane bado inaishi kwenye kijiji chenye wakazi 2,000, ambacho kinategemewa kuwa na shamla shamla nyingi siku ya kesho wakati ambapo kijana wao anatarajiwa kujaribu kuisaidia klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza kutwaa taji la sita Ligi ya Mabingwa mjini Kiev, katika dimba la Olympic.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 amehakikisha kijiji chake kinaweza kuiunga mkono timu yake katika mtindo tofauti, wakati ambapo wanatazamia kuwakabili mabingwa mara 12 wa michuano hiyo, Real Madrid.

"Kuna wakazi 2,000 kijijini. Nilinunua jezi 300 za Liverpool kwa ajili ya kuwatumia watu hao, hivyo mashabiki wanaweza kutazama mchezo wa fainali wakiwa wamevaa jezi hizo," Mane alikiambia chombo cha habari cha Uingereza.

Msenagali huyo hatarajii kurejea nyumbani hadi baada ya michuano ya Kombe la Dunia mwezi ujao nchini Urusi, lakini ana matumaini anaweza kuwapa zawadi mashabiki kwa kuendelea kuwasapoti.

"Hakuna mtu kijijini atafanya kazi katika siku hii (Jumamosi). Nitarejea kijijini kwenye majira ya joto baada ya Kombe la Dunia na nina matumaini nitaweza kuuonyesha medali kwa kila mtu."
Sadio Mane ametuma jezi 300 za Liverpool kijijini kwao Sadio Mane ametuma jezi 300 za Liverpool kijijini kwao Reviewed by Zero Degree on 5/25/2018 03:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.