Loading...

Manchester United yakamilisha usajili wa beki, Diogo Dalot kutoka FC Porto


Manchester United wamekamilisha usajili wa beki Diogo Dalot kutoka klabu ya FC Porto.
Nyota huyo mwenye umri wa maiaka 19, ambaye awali ilifahamika kuwa alikuwa na thamani ya karibu pauni milioni 17.4, alifanyiwa vipimo vya afya Manchester United siku ya Jumanne.

Dalot amesaini mkataba wa miaka mitano, kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine zaidi na anakuwa mchezaji wa pili kusainiwa na Jose Mourinho kwenye majira haya ya joto baada ya kiungo Mbrazil, Fred kutua Old Trafrod kwa pauni milioni 50.

Diogo Dalot 
Kwa mujibu wa taarifa ya Sky Sports, Mourinho alisema: "Diogo ni mchezaji chipukizi mwenye kipaji kikubwa sana kuja kuwa mchezaji mkubwa wa klabu hii kwa haraka sana. Ana sifa zote ambazo beki anastahiri kuwa nazo: kimaumbile, akili ya kiufundi na uwezo wake, ukijumuisha na mawazo ya academy ya Porto ambayo yanamwandaa mchezaji kwa ukomavu anohitaji katika ngazi za kitaalamu.

"Kwenye kundi la umri wake, ni beki bora zaidi wa pembeni barani Ulaya na tunaamini atakuwa na mafanikio makubwa sana Manchester United."
Dalot alisema: "Kujiunga na Manchester United ni kama ndoto kwangu mimi. Nimekulia katika academy ya Porto na ninashukuru sana kwa yote waliyonifanyia. Lakini nafasi ya kuja katika klabu kubwa zaidi duniani ni kitu ambacho siwezi kukiacha kipite.

"Ninashauku kubwa ya kufanya kazi na Jose Mourinho na kujifunza kila niwezacho kutoka kwa kocha mwenye mafanikio. Natazamia kucheza pamoja na wachezaji wakubwa kikosini."
Manchester United yakamilisha usajili wa beki, Diogo Dalot kutoka FC Porto Manchester United yakamilisha usajili wa beki, Diogo Dalot kutoka FC Porto Reviewed by Zero Degree on 6/06/2018 05:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.