Loading...

Ajali ya basi na treni ya mizigo yaua watu 10 Kigoma


Watu 10 wamefariki katika ajali iliyotokea baada ya basi la abiria lililogongana na treni eneo la Gungu katika manispaa ya Kigoma Ujiji, kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu, ajali hiyo ilitokea majira ya saa kumi na mbili na robo asubuhi.

Basi hilo la abiria ambalo linamilikiwa na kampuni ya Prince Hamida linadaiwa kugongana na treni lilipokuwa linatoka Kigoma Mjini kwenda Tabora.

Treni hiyo ya mizigo ilikuwa ikitoka Kazuramimba kwenda Kigoma Mjini.

Rais wa Tanzania John Magufuli ametuma salamu za rambirambi na kuwataka "wadau wote wa usalama barabarani kuchukua hatua madhubuti za kuzuia ajali hizi."

"Vyombo husika, chukueni hatua kali kwa wote wanaokiuka sheria za usalama barabarani," amesema.

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amesema eneo ilipotokea ajali hiyo hutokea ajali za aina hiyo mara kwa mara.

"Nimezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania ( TRC ) na tumekubaliana kuwa tuweke kizuizi ( barrier ) Katika eneo hili ambapo reli ikatiza barabara," amesema.

"Hii itasaidia sana kupunguza ajali za namna hii. Mkurugenzi wa TRC Bwana Masanja Kadogosa amekubali ushauri huu ambao Wananchi wengi wa Kigoma Mjini wamekuwa wakiutoa."
Ajali ya basi na treni ya mizigo yaua watu 10 Kigoma Ajali ya basi na treni ya mizigo yaua watu 10 Kigoma Reviewed by Zero Degree on 6/06/2018 04:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.