Loading...

Manchester United yakamilisha usajili wa Fred, Arsenal nayo yanasa beki mpya

Kiungo wa timu ya taifa ya Brazil, Fred
Klabu za Arsenal na Manchester United zinazoshiriki ligi kuu ya soka nchini England, zimekamilisha usajili wa kwanza kwa kila timu baada ya kuwatangaza nyota wawili waliotua kwenye timu hizo kwaajili ya matumizi ya msimu ujao.
Manchester United wametangaza kukamilisha usajili wa nyota wa Kimataifa wa Brazil anayecheza nafasi ya kiungo Frederico Rodrigues de Paula Santos maarufu Fred, kutokea klabu ya Shakhtar Donetsk.

Manchester United chini ya kocha Jose Mourinho inajaribu kuimalisha eneo la kiungo baada ya Nemanja Matic, kuonekana kushindwa kuendana na Paul Pogba hivyo matarajio yake kiungo Fred mwenye miaka 25 atamfaa.

Stephen Lichtsteiner 
Kwa upande wa Arsenal wao wametangaza usajili wake wa kwanza chini kocha mpya Unai Emery, baada ya kumsajili mlinzi wa kimataifa wa Switzerland, Stephen Lichtsteiner mwenye miaka 34. Mlinzi huyo ameondoka Juventus na kujiunga na Arsenal akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika.
Arsenal chini ya Unai Emery inaonekana kuanza kutafuta wachezaji wenye uzoefu hususani katika eneo la ulinzi baada ya walinzi wake Laurent Koscielny na Shkodran Mustafi kutofanya vizuri msimu uliopita.

Habari nyingeni kama hii:
Manchester United yakamilisha usajili wa Fred, Arsenal nayo yanasa beki mpya Manchester United yakamilisha usajili wa Fred, Arsenal nayo yanasa beki mpya Reviewed by Zero Degree on 6/05/2018 06:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.