Loading...

Baada ya kutolewa UEFA, Mourinho ashauriwa kumtema nyota huyu

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho
Jose Mourinho ameshauriwa aachane na Alexis Sanchez baada ya Manchester United kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa.

Manchester United walipewa nafasi kubwa ya kuweza kusonga mbele katika hatua ya robo fainali baada ya kupangwa na Sevilla kwenye hatua ya 16 bora. Timu hizo zilitoka sare ya 0-0, lakini United walitolewa nje ya michuano hiyo kwenye uwanja wao wa nyumbani kwa kuchapwa goli 2-1 siku ya Jumanne.

Alexis Sanchez
Hali ilizidi kuwa mbaya kwa Sanchez katika dimba la Old Trafford baada ya kuendelea kuonyesha kiwango cha kibovu kwenye mechi ya jana, huku Charlie Nicholas akisema kuwa nyota huyo hastahili kupewa nafasi katika kikosi cha Manchester United kwa sasa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Sky Sports, Nicholus alisema: “Mwanzoni mwa msimu, Manchester United walicheza kwa vizuri. Paul Pogba alikuwa na ari ya juu sana akiwa na Jesse Lingard nyuma yake pamoja na Romelu Lukaku ndani ya mchezo.”
“Ghafla, Sanchez anakuja, Marcus Rashford anaachwa nje na Anthony Martial anasahaulika, timu nzima inaanza kubadilika ili kuendana na Sanchez mchezoni.

“Kwa wakati huu, Sanchez hastahili kupewa nafasi ndani ya timu. Hilo ni suala binafi hilo na mara kwa mara anapoteza mpira.


“Nina uhakika mashabiki wengi wa Manchester United lazima watakuwa wanatazama na kusema “ni lini mtu huyu atatusaidia?” Ingawa anaonekana anajaribu kufanya vizuri, lakini hii ni Manchester United na unatakiwa kuonyesha mabadiliko katika mchezo mmoja baada ya mwingine na hafanyi hivyo.”
Baada ya kutolewa UEFA, Mourinho ashauriwa kumtema nyota huyu Baada ya kutolewa UEFA, Mourinho ashauriwa kumtema nyota huyu Reviewed by Zero Degree on 3/14/2018 08:49:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.