Loading...

Mgodi wa ACACIA kuilipa Serikali kodi ya dola za Kimarekani milioni 20 mwaka huu.


KAMPUNI ya Acacia Mining PLC imesema itailipa serikali kodi ya dola za Kimarekani milioni 20 mwaka huu baada ya kusainiwa mkataba wa maridhiano kati yake na Mamlaka ya Mapato (TRA) mwezi uliopita jijini Dar es Salaam.

Makubaliano hayo baina ya Acacia na TRA ni kilele cha mchakato uliofanywa kwa lengo la kuendeleza dhamira ya utendaji ya kampuni hiyo nchini Tanzania na kuongeza ushirikiano na wadau mbalimbali wa kampuni hiyo.



Alisema mkataba kati ya Acacia na TRA umetiwa saini na umetambuliwa na pande zote mbili kwamba hakuna kodi yoyote ya mapato yatokanayo na faida ambayo Acacia inastahili kulipa, haitalipwa.

Gordon alisema Acacia Mining ambayo iliingia nchini katika sekta ya madini ikijulikana kama Barrick na baadaye kama African Barrick Gold miaka 15 iliyopita, imekuwa ikitengeneza faida lakini haijarejesha mtaji iliowekeza wa dola za Kimarekani bilioni 3.8.

Hivi karibuni, Baraza la Rufaa za Kodi (TRAT), liliamua katika rufaa iliyokatwa na Acacia kwamba kampuni hiyo ilijenga mazingira ya kukwepa kodi ya dola za Marekani 41,250,426 (Sh bilioni 89) kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.




ZeroDegree.
Mgodi wa ACACIA kuilipa Serikali kodi ya dola za Kimarekani milioni 20 mwaka huu. Mgodi wa ACACIA kuilipa Serikali kodi ya dola za Kimarekani milioni 20 mwaka huu. Reviewed by Zero Degree on 4/11/2016 10:19:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.