Loading...

Hiki ndicho Modric alimwambia Neymar walipokuwa wanabadilishana jezi

Nyota wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar akibadilisha jezi na Modric wa Croatia
Luka Modric alimshauri Neymar aungane naye katika klabu ya Real Madrid baada ya kubadilishana jezi na mshambuliaji huyo kwenye mechi ya kirafiki kati ya Brazil na Croatia.

Nyota wa PSG, Neymar aling'ara kwenye mechi yake ya kwanza baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akiwa majeruhi kwa kuifungia Brazil goli la kuongoza kwenye mchezo uliomalizikwa kwa wao kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Croatia katika dimba la Anfield.

Neymar, ambaye alijiunga na PSG kwa ada iliyovunja rekodi ya pauni milioni 200 akitokea kwa mahasimu wa Real Madrid, Barcelona kwenye majira ya joto mwaka jana, alionekana akibadilishana na kusainiana jezi na Modric baada ya mchezo huo video ya tukio hilo ilirushwa hewani na shirikisho la soka nchini Brazil.

Huku kukiwa na uvumi mkubwa unaodai kwamba mshambuliaji huyo wa PSG ataondoka Ligue 1 kwenda kwa Mabingwa wa UEFA, Modric anaweza kuonekana akimwambia Neymar kuwa 'tunakusubiria', na kumfanya acheke na kuonyesha tabasamu.

Gazeti la Uhisapania, Marca liliripoti kwamba baba wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye ndiye wakala wake, Neymar Snr, aliiambia PSG kuwa mtoto wake alitaka kuondoka mapema iwezekanavyo, akisema kuwa alionana na wakurugenzi wa Real Madrid mjini Paris mwezi Disemba.

Neymar Jr
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez amekiri kuwa klabu yake ilitaka kumsajili Neymar kabla hajajiunga na Barcelona mwaka 2013 na amesema kuwa bado anatamani kumleta Mbrazil huyo Bernabeu.

Neymar alifunga magoli 28 na kusaidia ufungaji wa mabao mengine 16 kwenye michezo 30 ya michuano yote kwenye msimu wake wa kwanza akiwa na PSG kabla hajapata majeraha ya kifundo chake cha mguu Februari 25.
Hiki ndicho Modric alimwambia Neymar walipokuwa wanabadilishana jezi Hiki ndicho Modric alimwambia Neymar walipokuwa wanabadilishana jezi Reviewed by Zero Degree on 6/04/2018 08:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.