Loading...

Chelsea kuzipiku Arsenal, Liverpool kwa nyota huyu wa Ligue 1


Chelsea wanapigiwa upatu kuzipiku Arsenal na Liverpool kwa nyota huyu wa Ligue 1.

Chelsea wanafanya mazungumzo mazito kuwapindua wapinzani wao kwenye uhamisho unaotarajiwa kugharimu pauni milioni 43.9 wa nyota wa Bordeaux, Malcom.

Zote Chelsea na Liverpool ziko mbele ya Arsenal kwenye mbio hizo kwa kufanya mazungumzo yasiyo rasmi juu ya uhamisho wa kiungo mshambuliaji wa Bordeaux, Malcom kwenye majira haya ya joto.

Malcom
Kwa mujibu wa taarifa ya Sud-Quest, hivi karibuni wakala wa winga huyo wa Bordeaux, Malcom alisafiri na ndege kwenda Uingereza kuonana na Chelsea pamoja na Liverpool juu ya uwezekano wa raia huyo wa Brazil kuhamia Uingereza.

Chipukizi huyo kutoka Brazil huyo ni miongoni mwa viungo wenye uwezo mkubwa na kipaji cha kuvutia ambao wamekuwa wakizungumziwa katika siku za hivi karibuni.

Sawa na ilivyokuwa kwa Neymar kabla haiteka dunia kwa kujiunga na FC Barcelona mwaka 2013 na kisha kuvunja rekodi ya usajili kwa kujiunga na vigogo wa ufaransa, PSG kwenye dirirsha la usajili wa majira ya joto mwaka jana.

Ameonyesha uwezo ambao umezivutia klabu kadhaa barani Ulaya kama vile Liverpool, Chelsea, Arsenal, PSG, Bayern Munich na Manchester United.

Bordeaux wanaamini kwamba thamani yake ni karibu sawa na pauni milioni 43.9 na wangependelea kumuuza kwa dau kubwa kwenye dirisha hili la usajili.
Chelsea kuzipiku Arsenal, Liverpool kwa nyota huyu wa Ligue 1 Chelsea kuzipiku Arsenal, Liverpool kwa nyota huyu wa Ligue 1 Reviewed by Zero Degree on 6/04/2018 07:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.