Loading...

Mchezaji anayetarajiwa kuwa kivutio kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi

Kiungo wa timu ya taifa ya Costa Rica na klabu ya Deportivo La Coruna, Celso Borges
Mtoto wa kigogo na mpinga ngoma kwenye bendi... kiungo wa Costa Rica, Celso Borges anaweza kuwa kivutio zaidi kwenye Kombe la Dunia.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye anaichezea Deportivo La Coruna anatarajiwa kushiriki kwenye michuano ya pili ya Kombe la Dunia baada ya kuwa sehemu ya kikosi cha taifa lake kwenye michuano hiyo mwaka 2014 walipomaliza juu ya Uingereza, Italia na Uruguay kwenye kundi lao nchini Brazil mwaka 2014 kabla ya kufika robo fainali.

Golikipa wa Real Madrid, Keylor Navas na aliyekuwa winga wa klabu ya Fulham, Bryan Ruiz yanaweza kuwa majina yanayoweza kutambulika zaidi kwenye kikosi cha Costa Rica, lakini hakuna wachezaji wengi ambao wako Urusi ni wanachama wa bendi, wenye uwezo wa kuzungumza lugha nne na waliocheza moja ya mechi kubwa kwa kutumia jezi ya kuazima kutoka kwa shabiki. Soma zaidi kuona ni kwanini Borges anaweza kuwa kivutio cha wengi kwenye Kombe la Dunia Urusi…


Baba yake ni moja ya watu mashuhuri wa taifa kisoka
Alexandre Guimaraes alikuwa mkufunzi wa Costa Rica kwenye michuano miwili ya Kombe la Dunia
Baba yake na Borges ni, Alexandre Guimaraes, mmoja wa watu maarufu zaidi kisoka nchini Costa Rica.
Guimaraes alikuwa sehemu ya kikosi cha Costa Rica kilichofanikiwa kumaliza katika hatua ya 16 bora kwenye michuano yao ya kwanza ya Kombe la Dunia mwaka 1990 - Borges anauelezea ushindi wao dhidi ya Sweden kama "siku bora zaidi kwenye historia ya taifa" - na kisha aliendelea kuinoa timu walipofanikiwa kufuzu tena kwenye michuano hiyo mwaka 2002 na 2006.

Kuitwa kwa Borges mwaka 2014 na 2018 kuna maana kwamba aidha baba au mtoto ameshiriki kwenye kila Kombe la Dunia katika historia ya Costa Rica.

Kwa mujibu wa taarifa ya Sky Sports, Borges alisema: "Baba yangu ni sanamu yangu kubwa kwenye mpira wa miguu na maisha kwa sababu ya kila mafanikio aliyopata. Taifa halijashinda kitu chochote kikubwa lakini ni alama kwenye soka la Costa Rica."

Hata hivyo, Borges kufika robo fainali nchini Brazil inamaana ameipita rekodi ya baba yake ya Kombe la Dunia.

Ndoto yake ya kushiriki Olympic ilikatiswa na baba yake


Borges alikuwa sehemu ya Costa Rica U20, ambayo ilishiriki Michezo ya kufuzu kushiriki michuano ya Olympic mwaka 2007.

Celos Borges ni mchezaji mwenzake na Keylor Navas
Na walicheza dhidi ya Panama, ambao walikuwa chini ya uongozi wa baba yake kwa wakati huo.

Baada ya sare, mikwaju ya penalti ilihitajika kuwamua upande gani utaendelea na, kwa hofu, Borges alijitokeza kupiga mkwaju wa mwisho kwa Costa Rica.

Aliikosa penalti hiyo na kukiri kwamba, baada ya kuikosa penalti hiyo, hakuweza kutoa macho kwa baba yake, ambaye pia alishindwa kushangilia.

Miaka kadhaa baadaye, Borges alikiri kuwa "mkiwa, na kulia kwa siku kadhaa" - lakini alisahihisha makosa yake mwaka 2014 wakati alipofunga kwenye mikwaju katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia dhidi ya Ugiriki kuisaidia timu yake kusonga mbele.

Ni mpiga ngoma kwenye bendi


Borges ni shabiki mkubwa wa mziki wa miondoko ya rock huko Amerika - na pia ni mwanamuziki mwenye kipaji.

Na ujuzi wake nyuma ya ngoma unaweza kuonekana kwenye 'cover ya Toxicity' akiwa pamoja na mchekeshaji wa Peru na mwanamuziki Kurt Dyer - kipande cha video ambacho kimetazamwa karibu mara 125,000 Youtube.

Mziki wake haukuishia hapo aidha - aliungana na Dyer kwenye maonyesho ya kuchangisha fedha za kusaidi watoto wasiojiweza katika mgahawa wa Hard Rock Cafe katika mji wa San Jose, Costa Rica mwezi Juni 2017.

Borges aliruhusiwa kuchagua nyimbo zake anazozipenda zaidi na kuchagua kama Nirvana, Metallica, Foo Fighters, No Doubt, Pink Floyd na Guns and Roses.

Borges akishangilia kufika robo fainali kwenye Kombe la Dunia mwaka 2014
Alionyesha uwezo wake kwa zaidi ya saa moja na nusu na baba yake alikuwa sehemu ya watazamaji wa maonyesho hayo, ambayo yaliingiza maelfu kwa ajili ya kusaidia watoto wasiojiweza.

Licha ya kucheza mpira wa miguu mbele ya mashabiki zaidi ya elfu kumi, alikiri kuwa na woga baada ya "uzoefu mpya".

Anaweza kuzungumza lugha nne, lakini ni mpishi hatari


Vyombo vya habari nchini mwake vimemfananisha Borges "ubongo wa Costa Rica" - na ni kwa sababu nzuri.

Ukiachana na ngoma, alifundishwa kupiga kinanda na pia alipewa mafunzo ya mpira wa kikapu, karate, mpira wa wavu na riadha - ingawa mara nyingi alitoroka mafunzo hayo ili kwenda kucheza mpira wa miguu.

Borges anaweza pia kuzungumza lugha nne. Alizaliwa na kukulia Brazil hadi alipofikisha umri wa miaka 12 na hivyo anazungumza Kireno pia Kihispania - na pia alijifungza kiswidishi na kiingereza wakati alipokuwa Scandinavia.

Hata hivyo, sio mtu wa kuamini jikoni. Rafiki yake wa karibu, Renato Coto aliiambia La Nacion: "Sio mwangalifu, wakati mwingine anaposaidia kupika anajikata na kisu."

Aliwahi kucheza mechi akiwa amevaa shati ya shabiki


Borges alihusika kwenye tokio la aibu wakati anaichezea AIK ya Sweeden mwezi Agosti 2014.

Aliachwa nje ya kikosi kwenye Ligi ya Sweeden kilichosafiri kucheza na IFK Gothenburg baada ya klabu ya Evian ya Ufaransa kutoa ofa ya kutaka kumsajili.

Hakusafiri kwenda kufanya mazoezi pamoja na wachezaji wenzake kwa ajili ya mchezo huo mkubwa - lakini hilo lilisababisha matatizo wakati mkufunzi wa AIK, Andreas Alm alipobadili uamuzi wake dakika ya mwisho na kumuita kwenye kikosi cha kwanza.

Celos Borges anaichezea Deportivo ya Uhispania
Borges alipanda ndege kwenda Gothenburg - lakini mhusika wa jezi za klabu hakubeba jezi yake. Chaguo lake la pekee lilikuwa kwenda kuangaza kwenye vilabu kadhaa vya pombe pembeni ya uwanja kujaribu kutafuta jezi yoyote.

Kwa bahati nzuri, alijitokeza shabiki aliyekuwa na jezi yenye jina la Borges na namba 10 mgongoni, ambayo mchezaji huyo aliweza kuazima kwa ajili ya mechi hiyo.

Logo ya mdhamini ilishonwa haraka kwenye jezii hiyo, ambayo ilirejeswa kwa shabiki huyo, aliyejuliakana kwa jina la Luis, mwishoni mwa mchezo huo.

Borges alicheza dakika zote 90 akiwa na jezi ya shabiki, akaisaidia timu yake kushinda mabao 2-0. Uhamisho wake kwenda Evian uligonga mwamba na alicheza mechi nyingine 12 akiwa na AIK kabla hajajiunga na Deportivo mwezi Januari 2015.

"Tunatakiwa kumshukuru Luis kwa kumpa Celso nafasi ya kung'ara," alisema Alm (mkufunzi wa AIK) baada ya mechi.
Mchezaji anayetarajiwa kuwa kivutio kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi Mchezaji anayetarajiwa kuwa kivutio kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi Reviewed by Zero Degree on 6/09/2018 11:16:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.