Loading...

“Namfuatilia sana Diamond” - Mrema


Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustino Mrema amesema msanii wa Bongo Flava anayemfuatilia kwa sana ni Diamond Platnumz.

Ameeleza sababu ya kumfuatilia muimbaji huyo ni kutokana na kujituma kwake na muziki wake unavutia.

“Namfuatilia sana Diamond, ni kijana mdogo, muimbaji mahiri, yaani Diamond asaidiwe naona hatima yake katika maisha yake na nchi yetu atatufikisha mahali pazuri. Kwa muziki wake unakosha roho, hata sisi wazee, mimi naridhika sana,” Mrema ameiambia Times FM.

Katika hatua nyingine ametoa wito kwa serikali kuwa karibu zaidi na wasanii, hata hivyo amesema anaziona jitihada za Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe za kukutana na wasanii kila mara hasa pale wanapopata matatizo na kuwasaidia.
“Namfuatilia sana Diamond” - Mrema “Namfuatilia sana Diamond” - Mrema Reviewed by Zero Degree on 6/07/2018 11:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.