Loading...

Real Madrid, Liverpool kushindania saini ya nyota Chelsea

Wachezaji wa klabu ya Chelsea wakisherehekea kubeba taji la FA, 2018
Thibaut Courtois alirejea Chelsea kutoka Atletico Madrid mwaka 2014 baada ya kufurahia misimu mitatu akiwa Uhispania kwa mkopo. Tangu wakati huo amekuwa golikipa namba moja katika klabu hiyo na amejiendeleza hadi kufikia hatua ya kutajwa miongoni mwa magolikipa bora duniani.

Mbelgiji huyo anachukuliwa kama mmoja wa wachezaji wa muhimu katika klabu ya Chelsea na tayari ameshinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya Uingereza, moja la FA Cup na kombe la ligi moja. Alicheza mechi 46 akiwa na klabu msimu uliopita lakini walishindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa.

Lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 amekuwa akisita kusaini mkataba mpya pale Stamford Bridge na anaweza kuondoka kama mchezaji huru mwaka ujao wakati mkataba wake utakapokuwa umeisha. Amejiunga na kundi la wachezaji ambao hatima yao katika vilabu vyao iko shakani. Amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa kwenye usajili wa majira ya joto.

Thibaut Courtois
Kwa mujibu wa taarifa ya Gianluca Di Marzio, inaonyesha ni wazi kuwa Chelsea watamuuza Courtois kwenye majira haya ya joto, baada ya kuwa wameamua kusitisha mazungumzo ya makataba mpya. Wanataka kumuuza kuliko kumruhusu aondoke bure mwaka ujao, huku Liverpool na Real Madrid zikiwa kwenye harakati za kuisaka saini yake.

Liverpool wamekuwa sokoni kwa muda mrefu kwenye msako wa golikipa mpya. Simon Mignolet anatarajiwa kuondoka kwenye majira haya ya joto na Loris Karius amekuwa akionyesha kiwango cha kuvutia lakini makosa aliyofanya kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa yalionyesha klabu hiyo inahitaji kipa mwenye uwezo mkubwa zaidi.

Klabu hiyo inayonolewa na Jurgen Klopp imekuwa ikihusishwa na magolikipa wengi akiwemo na raia huyo wa Ubelgiji. Lakini inaoneka itakuwa ni vigumu kwa nyota huyo kujiunga na wapinzani wao kwenye EPL kama ataamua kuachana na washindi hao wa Kombe la FA.

Real Madrid pia wako kwenye msako wa golikipa mpya, ikiwa ni harakati za kusaka mrithi wa kudumu wa Keylor Navas. Lakini sio golikipa pekee ambaye amekuwa akihisishwa na vigogo hao wa La Liga.
Real Madrid, Liverpool kushindania saini ya nyota Chelsea Real Madrid, Liverpool kushindania saini ya nyota Chelsea Reviewed by Zero Degree on 6/01/2018 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.