Loading...

Simba yasonga mbele michuano ya SportPesa Super Cup


Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Simba wametolewa jasho naa Kariobangi Sharks ya Kenya kabla ya kuibuka mshindi kwa mabao 3-2 ya penalti.

Hii ni baada ya sare tasa katika mashindano ya kandanda ya SportPesa Super Cup kwenye uwanja wa Afraha mjini Nakuru eneo la Bonde la Ufa Jumatatu.

Nusra Papa hao wa Kariobangi wameze Simba lakini Jonas Mkude akawapatia mabingwa mara 19 wa ligi kuu ya Tanzania ushindi kwa kufunga bao muhimu lililowawezesha Wekundu wa Msimbazi kufuzu kwa nusu-fainali.

Sasa Simba watakutana na Kakamega Homeboyz ya Kenya Alhamisi wiki hii.

Jumanne AFC Leopards ya Kenya itajitosa uwanjani Afraha kupimana nguvu na Singiza FC ya Tanzania.

Endapo Leopards watashinda basi patachimbia Nakuru Alhamisi kwani Leopards watakutana na wapinzani wao wakuu Gor Mahia

Timu zingine ambazo tayari zimefuzu kwa nusu-fainali ni bingwa mtetezi Gor Mahia na Kakamega Homeboyz zote za Kenya.

Tofauti na matarajio ya wengi, Kakamega Homeboyz iliibandua mashindanoni timu kongwe nchini Tanzania Yanga kwa kuipachika mabao 3-1 kwenye mechi ya ufunguzi.
Matokeo hayo ni sawa na kumimina pilipili kwenye kidonda kibichi kwani ni hivi karibuni tu mahasimu wakuu wa Yanga, Simba walitwaa taji la ligi kuu ya Tanzania huku mashabiki wa Yanga wakibubujikwa na machozi wengine wakisema hiyo ni hujuma sasa.

Gor Mahia ilifuzu kwa nusu-fainali kwa kuizaba Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ya Zanzibar mabao 3-0.
Simba yasonga mbele michuano ya SportPesa Super Cup Simba yasonga mbele michuano ya SportPesa Super Cup Reviewed by Zero Degree on 6/04/2018 06:13:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.