Loading...

Kikosi cha wachezaji 23 watakoiwakilisha Ujerumani kwenye Kombe la Dunia, Sane nje!

Leroy Sane
Winga wa Manchester City Leroy Sane ameachwa nje ya kikosi cha mwisho cha Ujerumani ambacho kitawakilisha mabingwa hao watetezi Kombe la Dunia baadaye mwezi huu.

Sane, wachezaji wa Bayer Leverkusen Bernd Leno na Jonathan Tah na mshambuliaji wa Freiburg Nils Petersen wote wameachwa nje Joachim Low alipopunguza kikosi chake kutoka wachezaji 27 hadi 23.

Antonio Rudiger, Ilkay Gundogan na Mesut Ozil wamejumuishwa kikosini
Wachezaji watatu wa Ligi ya Kuu ya Uingereza waliojumuishwa ni beki wa Chelsea Antonio Rudiger, kiungo wa kati wa City Ilkay Gundogan na kiungo wa Arsenal Mesut Ozil wamo kikosini.

Ujerumani wamo Kundi F na Mexico, Sweden na Korea Kusini, na watacheza mechi yao ya kwanza mnamo Jumapili 17 Juni.

Sane alikuwa ameng'aa sana akichezea Manchester City kiasi kwamba alitawazwa mchezaji bora chipukizi wa mwaka Ligi ya Premia. Akiifungia City magoli 14 na kusaidia ufungaji wa mabao mengine 19.

Kikosi cha Ujerumani cha wachezaji 23:

Walinda lango: Manuel Neuer (Bayern Munich), Marc-Andre ter Stegen (Barcelona), Kevin Trapp (Paris St-Germain)

Mabeki: Jerome Boateng (Bayern Munich), Matthias Ginter (Borussia Monchengladbach), Jonas Hector (Cologne), Mats Hummels (Bayern Munich), Joshua Kimmich (Bayern Munich), Marvin Plattenhardt (Hertha Berlin), Antonio Rudiger (Chelsea), Niklas Sule (Bayern Munich)

Viungo wa kati: Julian Brandt (Bayer Leverkusen), Julian Draxler (Paris St-Germain), Leon Goretska (Schalke), Ilkay Gundogan (Manchester City), Sami Khedira (Juventus), Toni Kroos (Real Madrid), Mesut Ozil (Arsenal), Sebastian Rudy (Bayern Munich)

Washambuliaji: Mario Gomez (Stuttgart), Thomas Muller (Bayern Munich), Marco Reus (Borussia Dortmund), Timo Werner (RB Leipzig)
Kikosi cha wachezaji 23 watakoiwakilisha Ujerumani kwenye Kombe la Dunia, Sane nje! Kikosi cha wachezaji 23 watakoiwakilisha Ujerumani kwenye Kombe la Dunia, Sane nje! Reviewed by Zero Degree on 6/04/2018 04:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.