Chadema 'wamkaba koo' msemaji wa Rais
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa |
Hayo yamewekwa bayana na taarifu zilizotolewa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje- CHADEMA, John Mrema mchana wa leo Juni 04, 2018 baada ya kupita siku kadhaa tokea kulipomalizika vikao vya Halmashauri Kuu Taifa ya CCM vilivyofanyikia ndani ya kumbi za mikutano zilizopo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
"Tarehe 21 Mei, 2018 ilitolewa taarifa ya Ofisi ya Rais Ikulu ikiwa imesainiwa na Gerson Msigwa kuhusu tukio la Mwenyekiti wa CCM Taifa, John Pombe Magufuli kupokea taarifa ya ukaguzi wa mali za CCM katika Makao Makuu ya Chama hicho Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Kwa mara nyingine tena tarehe 25 Mei, 2018 Msigwa kwa kujua au kutojua au kwa kiburi cha malamka alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwa nafasi yake kama Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu kuhusu uteuzi wa Wajumbe wawili wa Halmashauri Kuu ya CCM uliofanywa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa John Pombe Magufuli", amesema Mrema.
Aidha, Mrema amesema kwa mujibu wa Katiba ya nchi Ibara ya 3(1) imetamka wazi kuwa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na ni nchi ya mfumo wa vyama vingi vya siasa huku Kanuni maadili ya vyama vya siasa za mwaka 2007, Kanuni ya 5(1) inakataza chama chochote cha siasa kutumia mamlaka, rasilimali za serikali kwa kujinufaisha kisiasa.
"Gerson Msigwa kama Mtumishi wa Umma mwenye wadhfa wa Mkurugenzi kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 anatakiwa na anapaswa kuzingatia masharti ya Viongozi wa umma. Kifungu cha 21 cha sheria hiyo kinakataza kiongozi wa umma kutumia mali za serikali isivyoruhusiwa..
Kwa kuwa Msigwa ameendelea kunukuliwa akisisitiza kuwa yeye ni Msemaji wa Rais na ambaye ni Mwenyekiti wa CCM huku akijua kufanya hivyo ni kukiuka masharti kama tulivyoeleza, sisi kama Chama cha siasa tutachukua hatua kwa hilo", amesisitiza Mrema.
Pamoja na hayo, Mrema ameendelea kwa kusema "tunamtaka Msajili wa Vyama vya Siasa kutumia mamlaka yake kupitia Kanuni ya 6(1)(d) ya Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa kutoa tamko dhidi ya ukiukwaji wa Kanuni hizo uliofanywa na CCM kwa kutumia mali za umma kwa maslahi yao ya kisiasa. Msajili akishindwa kufanya hivyo tutawasilisha malalamiko rasmi kwake kwa mujibu wa Kanuni ya 6(1)(a) kuhusu ukiukwaji huo.
Tunamtaka Katibu Mkuu Kiongozi au Tume ya Utumishi wa Umma kama mamlaka za nidhamu kumchukulia hatua Gerson Msigwa kwa kukiuka masharti ya Utumishi wa Umma kwa kufanya siasa wakati wa masaa ya kazi na pia kujipa nafasi ya kuwa Msemaji wa CCM huku akijua Chama hicho kina Msemaji wake".
Kwa upande mwingine, Mrema amesema endapo hayo yote hayatofanywa na mamlaka husika zilizotajwa basi wao watachukua hatua zaidi juu ya jambo hilo ambalo linatendwa kinyuma na taratibu.

Reviewed by Zero Degree
on
6/04/2018 02:05:00 PM
Rating: