Loading...

Singida United yaungana na Simba nusu fainali SportPesa Super Cup


SINGIDA United imeungana na Simba kuingia hatua ya nusu fainali ya mashindano ya SportPesa Super Cup kwa ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya AFC Leopards wa njia ya matuta.

Kikosi cha Singida United
Ushindi huo umepatikana na kuiwezesha Singida United kutinga hatua hiyo baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 0-0.

Kipa wa Singida, United, Manyika Junior, ameibuka shujaa wa mchezo huo baada ya kuokoa penati mnamo kipindi cha pili kabla ya dakika 90 hazijamalizika.

Matokeo yanaifanya Singida iungane na Simba huku Yanga na JKU kutoka Tanzania zikiwa tayari zimeshaaga mashindano.

Lakini Leopards watajilaumu wenyewe kwani mchezaji wao wa kiungo Whyvonne Isuza alishindwa kufunga penalti katika kipindi cha pili.

Kikosi cha AFC Leopards
Leopards wanajiunga na Yanga ya Tanzania, JKU ya Zanzibar na Kariobangi Sharks ya Kenya ambao tayari wameng'olewa mashindanoni.

Fainali ni Jumapili, na mshindi atasafiri England mwezi ujao kupambana na Everton.

Singida itakutana na bingwa mtetezi Gor Mahia Alhamisi wiki hii kwenye nusu-fainali, huku Simba ikimenyana na Kakamega Homeboyz. Timu mbili za Kenya na Tanzania ndizo zimefuzu kwa nusu-fainali.
Singida United yaungana na Simba nusu fainali SportPesa Super Cup Singida United yaungana na Simba nusu fainali SportPesa Super Cup Reviewed by Zero Degree on 6/05/2018 06:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.