Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 6 Juni, 2018

Moses Simon
Liverpool wanafikiria kujaribu kumsajili nyota wa timu ya taifa ya Nigeria, Moses Simon, kwa mujibu wa taarifa ya Liverpool Echo.

Leicester wameanzisha mazungumzo na beki wa klabu ya West Brom, Jonny Evans, ambaye amekata tamaa ya uhamisho kwenda Manchester City.

Manuel Pellegrini yuko kwenye mgogoro na uongozi wa klabu ya West Ham - zikiwa zimepita wiki mbili tu, tangu ataeuliwe.

Wakala wa Yaya Toure amedai kuwa kiungo huyo yuko tayari kuichezea klabu nyingine kubwa kwa mshahara wa pauni 1 kwa wiki.

Manchester City wanatafakari juu ya kumtoa Oleksandr Zinchenko kwa Napoli kama sehemu ya ofa ya kumsajili Jorginho.

RB Leipzig wanajaribu kumsajili Ademola Lookman moja kwa moja kutoka Everton.

Daniel Stendel anatarajiwa kuteuliwa kuwa meneja mpya wa Barnsley.

Brighton watatoa ofa ya pauni milioni 5 kwa Sunderland kumsajili kiungo wa klabu hiyo, Paddy McNair. (Mirror)

Rodrygo, 17
Real Madrid na Barcelona watashindana kumsajili winga kutoka Brazil, Rodrygo, ambaye anaichezea klabu ya Santos. 

Liverpool wamethibitisha kuwa Pepjin Lijnders amerejea kwenye kibarua cha ukunzi kwenye benchi la ufundi la timu ya wakubwa ya klabu hiyo. (Marca)

Bernd Leno yuko huru kuondoka Bayer Leverkusen, kwa mujibu wa mkurugenzi wa kandanda wa klabu hiyo, Rudi Voller, lakini ni ikiwa kama utaratibu wa klabu utafuatwa. (Bild)

Arsenal wanatarajia kufwatisha usajili wa Stephan Lichtsteiner kwa kuthibitisha usajili beki wa Borussia Dortmund, Sokratis anayetarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya katika klabu hiyo ya Uingereza wiki hii. (Kicker)
 
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, Maurcio pochettino bado ni kinara kwenye orodha ya wagiombea wa nafasi ya meneja Real Madrid, na meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp pia ameingizwa kwenye orodha hiyo.

Willian anakiri kuwa na wakati mgumu alipokuwa anaanzia benchi katika klabu ya Chelsea msimu uliopita, lakini anasema kuwa anaheshimu uamuzi wa Conte.

Mshambuliaji wa Celtic, Nadir Ciftic ataondoka katika klabu hiyo ya Uskoti mwishoni mwa mwezi Juni.

Diogo Dalot
Manchester United wamekamilisha usajili wa beki kutoka klabu ya FC Porto, Diogo Dalot kwa mkataba wa miaka mitano. (Sky Sports)

Manchester United wanaweza kugeuzia macho yao kwenue usajili wa Toby Alderweireld baada ya kumsajili Fred.

Antonio Conte anakabiliwa na tishio la kusubiri kwa muda mrefu zaidi kujua juu ya hatima yake katika klabu ya Chelsea wakati Real Madrid ikiendelea kusaka meneja mpya.

Stoke City wako kwenye mazungumzo zaidi na nyota kutoka Wales, Joe Allen juu ya mkataba mpya.

Jack Butland na Danny Rose wanakaribia kufikia hatua ya kuwa na namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza Kombe la Dunia. (Telegraph)

Mkurugenzi mpya wa kandanda katika klabu ya Everton, Marcel Brands, amesema Farhad Moshiri hatakuwa na matumizi mengine makubwa ya fedha kwenye majira haya ya joto na matumizi makubwa ya fedha kwenye kulipa mishahara lazima yapunguzwe. (Guardian)
 
Tottenham wanapanga kujaribu kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial wiki ijayo.

Fulham wamewakasirisha mashabiki kwa kutangaza ongezeko kubwa kwenye bei za teketi za msimu.

Jordan Henderson akiwa na meneja wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate
Gareth Southgate alimwambia Jordan Henderson kuwa alipoteza nafasi kwenye mbio za kuwania Unahodha wa timu ya taifa ya Uingereza kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa. (Daily Mail)

Juventus wameripotiwa kuikataa ofa ya pauni milioni 50 kutoka Manchester City kwa ajili ya kiungo wa klabu hiyo ya Serie A, Miralem Pjanic.

Manchester City wanaweza kuingiza pauni milioni 148 kama watatawala michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Jamie Vardy atapewa nafasi ya kupigania nafasi kwenye kikosi cha kwanza kwenye mchezo wao dhidi ya Costa Rica.

Leicester wako kwenye nafasi nzuri ya kufanikisha usajili wa nyota wa klabu ya Norwich, James Maddison.

Stoke City wanapanga kutoa ofa ya kushangaza ya pauni milioni 14 kwa ajili ya straika wa klabu ya Watford, Andre Gray. (Sun)

Arsenal wameambiwa watalazimika kulipia pauni milioni 35 kwa ajili ya kiungo wa klabu ya Sevilla, Steven N'Zonzi kwenye majria haya ya joto. (Express)

Mbia wa New York Yankees, Peter B Freund anaandaa ofa ya kuinunua klabu ya Aston Villa kwa pauni milioni 75.

Benik Afobe
Wolves wanatarajia kuingiza pauni milioni 2 kabla ya wiki kuisha kwa kumuuza  Benik Afobe kwenda Stoke City. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 6 Juni, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 6 Juni, 2018 Reviewed by Zero Degree on 6/06/2018 10:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.