Loading...

Canada ya pili kuhalilisha matumizi ya bangi kwa starehe


Canada imekuwa nchi ya pili duniani baada ya Uruguay kuhalilisha uuzaji, umiliki na matumizi ya bangi kwa starehe.

Soko la kitaifa la uuzaji wa bangi lilifunguliwa saa sita usiku kuamkia Jumatano huku kukiwepo maswali kuhusu madhara kwa afya , sheria na usalama wa umma.

Matayarisho ya kuhalilishwa matumizi ya mihadarati hiyo ilijumuisha kutumwa kwa sanduku la posta sheria kwa wakaazi milioni 15 inayoeleza sheria mpya na kampeni ya uhamasisho wa umma.

Lakini wasiwasi bado unasalia, ikiwemo utayari wa idara ya polisi kukabiliana na visa vya uendeshaji magari, madereva wakiwa wamelewa bangi.

Majimbo na manispaa nchini Canadian yamekuwa yakijitayarisha kwa miezi kadhaa kuelekea kumalizika kwa sheria inayopiga marufuku bangi nchini.

Tawala za kieneo zinatarajiwa kutoa muongozo kuhusu sehemu ambazo bangi itauza na inapoweza kutumiwa.

Hili limezusha kazi kubwa kisheria nchini huku idara zikichagua mifumo isiyobana uuzaji na matumizi ya bangi.

Wanunuzi wa kwanza kufika bangi halali muda mfupi baada ya saa sita usiku
Maduka yalifunguliwa ilipofika saa sita usiku na katika baadhi ya maeneo tayari kulikuwa na misururu ya watu waliosubiri kuhudumiwa.

Katika baadhi ya maeneo tayari kulikuwa na misururu ya watu waliosubiri kuhudumiwa.
Ontario, jimbo lenye idadi kubwa ya watu nchini Canada litaanza kufunguwa maduka ya kuuza msimu ujao wa machipuko, licha ywa kwamba wateja wataweza kununua bangi kupitia maduka ya mitandaoni.

Baadhi ya maduka ambayo yamekuwa yakiuza bangi kiharamu ambayo yameshamiri katika miaka ya nyuma tangu kupendekezwa kwa sheria hiyo huenda pia yakasalia wazi.

Haijulikani wazi iwapo Polisi itawasaka mara moja au iwapo itawapuuzia tu na kuwaruhusu waendelee na shughuli hizo.

Ni kwanini Canada imehalilisa bangi?


Kuhalilishwa kwa bangi kunatimiza ahadi aliyotoa waziri mkuu Justin Trudeau, katika kampeni ya uchaguzi mnamo mwaka 2015.

Kiongozi huyo wa chama tawala cha ki Liberali ameeleza kwamba sheria za jadi za nchi hiyo dhidi ya matumizi ya bangi hazifanyi kazi, ukizingatia kwamba raia nchini humo ni miongoni mwa wanaotumiwa kwa kiasi kikubwa bangi duniani.

Ameeleza kuwa sheria hiyo mpya imeundwa kuwaondolewa watoto bangi karibu, na kuondosha faida wanayoipata wahalifu.

Serikali ya shirikisho inakadiria pia itapata $ milioni 400 kwa mwaka katika tozo la kodi katika mauzo ya bangi.

Umiliki wa bangi ulikuwa haramu kwa mara ya kwanza Canada mnamo 1923 lakini matumizi yake kwa misingi ya dawa ilihalilishwa tangu 2001.

Canada inafuata nyayo za Uruguay, iliyokuwa nchi ya kwanza duniani kuhalilisha uuzaji wa bangi kwa starehe mnamo 2013.

Baadhi ya majimbo nchini Marekani tayari yamepiga kura kusitisha marufuku hiyo.

Matumizi ya bangi kwa manufaa ya dawa yamekuwa yakikithiri pia katika nchi nyingi za Ulaya.

Source: BBC
Canada ya pili kuhalilisha matumizi ya bangi kwa starehe Canada ya pili kuhalilisha matumizi ya bangi kwa starehe Reviewed by Zero Degree on 10/17/2018 07:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.