Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 28 Octoba, 2018

Dele Alli, 22
Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya England and Tottenham, Dele Alli anakaribia kusaini mkataba mpya klabuni hapo. (Sky Sports)

Meneja wa zamani wa Chelsea manager Antonio Conte na kocha wa Juventus Max Allegri wametajwa kuwa wale wanaweza kuchukua nafasi yake Jose Mourinho kama meneja wa Manchester United mwaka ujao. (Express)

Manchester City huenda wakawapiku Tottenham katika kumwinda kiuungo wa kati wa Ajax Frenkie de Jong, 21.

Arsenal watajaribu kumsajili kiungo wa kati wa klabu ya Manchester United, Juan Mata ikiwa Mhispania huyo mwenye miaka 30 ataondoka bila mkataba msimu ujao. (Star)

Juventus wanataka kumrudisha Paul Pogba kwenye klabu na watatoa ofa kwa mchezaji huyo mwenye miaka 25 kiungo wa kati wa Manchester United mwezi January. (Tuttosport)

Manchester United wamemuamrisha Pogba aache kuzungumzia matatizo yake na meneja wa klabu hiyo, Jose Mourinho na uwezekano wake wa kuondoka Old Trafford. (Mirror)

Napoli wamesema kuwa hawatasikiliza ofa zilizo chini ya pauni milioni 80 kwa mshambuliaji mwenye miaka 27 raia wa Italia Lorenzo Insigne anayehusishwa na Liverpool. (Gazetta dello Sport)

Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Eric Cantona anasema anateseka kuona klabu yake ya zamani ikicheza chini ya usimamizi wa Jose Mourinho na angependa kuona mchezaji wa zamani wa United akichukua nafasi ya Mreno huyo. (Manchester Evening News)

Anthony Martial
Mshambuliaji wa Ufaransa, Anthony Martial amekataa mkataba mpya aliopewa na Manchester United.

Mshambuliaji wa Leicester Jamie Vardy, 31, amemkasirikia Meneja wake Claude Puel,ambaye anadaiwa kuwa alimuondoa kutomjumuisha mchezaji huyo katika mchezo leo jumamosi dhidi ya West Ham. (Telegraph)

Baadhi ya wachezaji wa Manchester United wanaweza kupigwa faini na klabu yao baada ya kukataa kuhudhuria hafla iliyoandaliwa na mfadhili wao ya kuandamana dhidi ya tatizo la usafiri ambao timu iliwahi kukabiliana nao katika mashindano ya ligi.

Wakati huohuo Bosi wa United Jose Mourinho anataka wachezaji wake wajumuike naye kutembea kutoka Hotelini mpaka Uwanjani Old Traford kukwepa foleni inayoweza kutokea kama ilivyotokea kwenye mchezo dhidi ya Juventus kwenye UEFA ingawa watu wa usalama nchini humo wamepinga zoezi hilo. (Mail)

Tottenham imepanga kumsainisha mchezaji wa Brazil Malcom, 21,wa Barcelona ambaye anahangaikia kuchukua nafasi ya Philippe Coutinho na Ousmane Dembele. (Corriere dello Sport)

Kiungo wa kati Mousa Dembele, 31 yuko katika orodha ya juu ya wachezaji wa Tottenham ambao meneja Mauricio Pochettino anataka kuwauza katika kipindi hiki cha kiangazi. (Sun)

Aaron Ramsey
Kiungo, Aaron Ramsey amejihudhuru ili aondoke timu ya Arsenal katika kipindi cha kiangazi, ingawa amesema kuwa anashangaa kwanini Arsenal wamesitisha tena mkataba wake wa miaka minne (Evening Standard)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 28 Octoba, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 28 Octoba, 2018 Reviewed by Zero Degree on 10/28/2018 10:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.