Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 1 Novemba, 2018

Malcom
Malcom amekanusha uvumi unaodai kuwa yuko anatafuta uwezekano wa kuondoka Barcelona mwezi Januari. (Express)

Borussia Dortmund inaongoza kichang'anyiro cha kuwania saini ya kiungo wa Manchester City, Phil Foden.

Jack Wilshere ana matumaini ya kurejea mwishoni mwa mwezi Novemba baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa kifundo cha mguu.

Shirikisho la soka nchini Uingereza, FA lina hamu ya kumpata mbadala wa mkurugenzi wa kandanda Dan Ashworth, ambaye anajiunga na klabu ya Brighton mwaka ujao. (Daily Mail)

Chelsea wako makini na sakata la mkataba wa Declan Rice katika klabu ya West Ham.

Kiungo wa klabu ya Brighton, Pascal Gross anakabiliwa na ongezeko la muda wa kuendelea kukaa benchi baada ya kujitonesha majeraha yake.

Ben Coker amekuwa mchezaji wa tatu kutoka Southend kupata majeraha yatakayomweka hatarini kukosa msimu mzima ndani ya wiki moja. (Star)

Chipukizi wa klabu ya Manchester City, Brahim Diaz yuko tayari kujiunga na Real Madrid kama mchezaji huru kwenye majira ya joto.

Real Madrid wanataka kufanya mazungumzo na Roberto Martinez mapema zaidi, huku kocha huyo wa Ubelgiji akiongoza orodha ya wanaopigiwa upatu kurithi mikoba ya Julen Lopetegui Bernabeu. (Telegraph)

Juan Mata
Juventus wana hamu ya kumnasa Juan Mata, huku hofu juu ya hatima ya Mhispania huyo katika klabu ya Manchester United ikiendelea kukua.

Mshabuliaji wa klabu ya Manchester United, Alexis Sanchez anawaniwa na Paris Saint-Germain kwenye usajili utakaoshitukiza katika kipindi kijacho cha majira ya joto. (Sun)

Juan Mata anahudumia mmsimu wa mwisho wa mkataba wake katika na klabu ya Manchester United.

Kiungo wa Kati wa Denmark Christian Eriksen, 26, anajiandaa kutia saini kandarasi ya kurefusha muda wake Tottenham. (Evening Standard)

Brahim Diaz anakataa kusaini mkataba mpya Manchester City na anaweza kutima Etihadi kama mchezaji huru kwenye majira ya joto mwakani.

Manchester United ilikasirishwa na lugha chafu iliyotumiwa na kiungo wa kati wa Liverpool na England Jordan Henderson, 28, na wametumia hilo kujitetea kwenye rufaa yao kwa FA kumhusu meneja wake Jose Mourinho.

Aliyekuwa meneja wa Rangers, Mark Warburton na aliyekuwa mkurugenzi wa michezo wa Manchester City, Mike Rigg ni miongoni mwa majina manne yanaoongza katika orodha ya wagombea wa nafasi ya mkurugenzi wa michezo wa FA. (Times)

Loris Karius
Mkataba wa mkopo wa miaka miwili wa Kipa wa Liverpool, Loris Karius katika klabu ya Besiktas hautavunjwa licha ya tetesi zinazodai klabu hiyo ya Uturuki inataka kumrejesha Anfield mchezaji huyo mwezi Januari. (Liverpool Echo)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 1 Novemba, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 1 Novemba, 2018 Reviewed by Zero Degree on 11/01/2018 07:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.