Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 3 Novemba, 2018
![]() |
| Harry Kane |
Straika wa Tottenham na Uingereza, Harry Kane bado analengwa na klabu ya FC Barcelona kama mbadala wa Luis Suarez, 31.
Manchester City walikuwa tayari kukidhi vigezo vya kuvunja mkataba wa Lionel Messi, uliokuwa na thamani ya pauni milioni 250 kabla nyota huyo hajasaini mkataba mpya mwaka jana. (Mundo Derpotivo)
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anatumai kwamba mshambuliaji wa klabu hiyo, Antony Martial atabakia Old Traford.
Nyota wa zamani wa Arsenal, Nicklas Bendtner amehukumiwa kifungo cha siku 50 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumjeruhi dereva taxi.
Ryan Giggs anaamini kwamba Aaron Ramsey anaweza kucheza katika klabu yoyote ile.
Mauricio Pochettino anaamini kuwa wachezaji wa Tottenham wanasini mikataba mipya kwa sababu ya mapenzi kwa klabu yao na si kwa sababu yake.
Maurizio Sarri anaamini Chelsea inahitaji kuimarisha safu ya ulinzi ili kuendana na mikiki ya Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu. (Sky Sports)
Manchester City watishia kuishtaki UEFA kwa lengo la kuepuka kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa.
Manchester United wako tayari kukubali ofa itakayowafikia kwa ajili ya Ander Herrera mwezi January. (Sun)
![]() |
| Vichai Srivaddhanaprabha |
Meneja wa Leicester, Claude Puel amewaambia wachezaji wake kwamba yeyote ambaye hayuko tayari anaweza kujiondoa kwenye mchezo wao dhidi ya Cardiff.
Meneja wa Everton, Marco Silva amekiri kwamba washambuliaji wake wanahitaji kupewa maelekeza zaidi.
Jurgen Klopp anaamini vita ya kuwania ubingwa msimu huu inaweza kuisha vizuri kwa upande wao. (Guardian)
Manchester City inatazamia kumsajili nyota wa Lyon, Tanguy Ndombele kama mbadala wa Fernandinho.
Chelsea wanatumai kwamba, hali ya sintofahamu katika nafasi ya meneja Real Madrid inaweza kuwasaidia kumbakisha Eden Hazard. (Telegraph)
Manchester City walificha kiasi cha pauni milioni 30 ili wakaguzi kutoka UEFA FFP wasikione, nyalaka zilizovuja zimeonyesha.
Bernd Leno anatarajiwa kushinda mbio za kuwania nafasi ya kuanza na kikosi cha kwanza cha Arsenal dhidi ya Liverpool mbele ya Petr Cech. (Daily Mail)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 3 Novemba, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
11/03/2018 07:20:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
11/03/2018 07:20:00 AM
Rating:


