Wema aachiwa kwa dhamana, kesi yaahirishwa hadi Novemba 20
Wema amesomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mahira Kasonde ambapo amekana kosa hilo kisha kuachiwa kwa dhamana ya Sh. milioni 10 kupitia kwa Salim Limu.
Aidha, Wema ambaye alikuwa akiwakilishwa na wakili Reuben Simwanza, ametakiwa asiposti video au picha yoyote isiyo na maadili au inayoashiria ngono kwenye mitandao.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 20, mwaka huu.
Akizungumza baada ya kesi hiyo kuahirishwa, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Kudhibiti Mawasiliano nchini (TCRA) Johannes Karungura amesema:
“TCRA tupo makini, tunapenda kuwatahadharisha wale wote waliokuwa na picha na video za namna hiyo wazifute katika simu zao, kwa sababu haziruhusiwi.”
“TCRA tupo makini, tunapenda kuwatahadharisha wale wote waliokuwa na picha na video za namna hiyo wazifute katika simu zao, kwa sababu haziruhusiwi.”
Wema aachiwa kwa dhamana, kesi yaahirishwa hadi Novemba 20
Reviewed by Zero Degree
on
11/01/2018 01:35:00 PM
Rating: