Loading...

Zlatan Ibrahimovic atwaa tuzo hii MLS


Mshambuliaji wa LA Galaxy, Zlatan Ibrahimovic ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mwaka ya mchezaji bora mpya katika MLS kwa mwaka 2018.

Nyota huyo wa zamani wa Manchester United amefurahia msimu wake wa kwanza Marekani, akifunga magoli 22 na kutoa 'assist' 10 katika mechi 27.

Licha ya mchango wake mkubwa, Galaxy bado walishindwa kufuzu hatua ya mtoano MLS baada ya kumaliza katika nafasi ya saba kwenye michuano ya Western Conference, pointi moja nyuma ya Real Salt Lake.

Ibrahimovic alimaliza mbele ya Wayne Rooney kwenye uchaguzi huo
Tuzo hiyo, ambayo ni maalum kwa wachezaji wenye uzoefu lakini ambao hawajawahi kushiriki Ligi ya MLS, inapigiwa kura na wachezaji, vilabu na vyombo vya habari.

Ibrahimovic alijipatika wastani wa asilimia 36.36 ya kura zote, mbele ya nyota wa DC United, Wayne Rooney (asilimia 32.25) na mshambuliaji wa Los Angeles FC, Carlos Vela (asilimia 13.47). Mshambuliaji wa zamani wa Derby County - ambaye kwa sasa Sporting Kansas City - Johnny Russell alipata asilimia 2.51 ya kura.

Ibrahimovic, Rooney na Vela wote kwa pamoja walijumuishwa kwenye kikosi cha mwaka cha MLS.
Zlatan Ibrahimovic atwaa tuzo hii MLS Zlatan Ibrahimovic atwaa tuzo hii MLS Reviewed by Zero Degree on 11/13/2018 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.