Clouds yatangaza tarehe na sehemu itakayofanyika Fiesta baada ya kuahirishwa
Ikumbukwe kwamba Fiesta ilifanyika karibia mikoa 15 nchini Tanzania lakini ilipofika zamu ya Dar Es Salaam ambayo ndio ilikuwa inafunga msimu mpya wa Fiesta ilisitishwa kwa madai kwamba sehemu ambako ingeenda kufanyika ingeleta taharuki kutokana na kelele zitakazojitokeza mahala hapo.
Uongozi wa CGM umetangaza tarehe mpya na sehemu ambako Tamasha hilo litafanyika.
"Tarehe 22 Disemba kwenye Viwanja vya Posta DSM, Machampion wote wa nchi wanakwenda kutoa shukrani moja kubwa na kushangalia mafanikio ya mwaka huu.
Ni mara 2 ya tulichokimiss: stage ya viwango, sound kubwa kuliko, bata la kihistoria na list ndefu ya machampion. . #TigoFiesta2018 ".Wameandika Clouds Media.
Clouds yatangaza tarehe na sehemu itakayofanyika Fiesta baada ya kuahirishwa
Reviewed by Zero Degree
on
12/12/2018 08:35:00 AM
Rating: