Loading...

Sina uadui na Mbunge yeyote - Mtolea


Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa tiketi ya CUF, Abdallah Mtolea amesema licha ya kujiuzulu kwenye nafasi yake bado ana mahusiano mazuri na waliokuwa wabunge wenzake wa upinzani na kusisitiza kuwa mahusiano hayo yatazidi kuendelea.

Kwa mubjibu wa taarifa ya Eatv, Mtolea alisema: "Mimi sina uadui na Mbunge yeyote, kwa kifupi wabunge wa vyama vyote ni marafiki zangu, kuhusu kama wanahofu kwamba ukaribu wangu nitakuwa nikiwashawishi wabunge wengine wahame mimi siwezi kuwasemea."

"Kuhusu suala la nani atakuwa mpinzani wangu kwenye uchaguzi wa marudio bado sijajua maana mimi bado sijapitishwa kugombea tena na uteuzi utafanyika disemba 20," ameongeza.

Mtolea amedai siasa haina udaui na kwamba wabunge wote ni watu ambao amekuwa akishirikiana nao kila siku.

Novemba 15 mwaka huu, Abdallah Mtolea alitangaza kujivua nafasi yake ya Ubunge na kwa kile alichokidai kuchoshwa na mgogoro uliokuwa ukiendelea kwenye Chama cha Wananchi CUF ambapo baadaye altangaza kujiunga Chama Cha Mapinduzi CCM.
Sina uadui na Mbunge yeyote - Mtolea Sina uadui na Mbunge yeyote - Mtolea Reviewed by Zero Degree on 12/12/2018 08:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.