Kauli ya Guardiola kuhusu mbio za ubingwa EPL baada ya kuchapwa 2-0 na Chelsea
Goli la pili la N'golo Kante msimu huu liliwapa Chelsea nafasi ya kuongoza mchezo |
Magoli ya N’Golo Kante na David Luiz yaliipa Chelsea ushindi wa 2-0 Stamford Bridge jana. Waliipa Manchester City kichapo cha kwanza kwenye EPL tangu April wakati walipochapwa 2-3 na Manchester United katika uwanja wao wa Etihad. City sasa wanashuka nafasi ya pili kwenye msimamo wa EPL na wako nyuma ya Liverpool kwa alama moja.
Alipoulizwa kuhusu mbio za ubingwa, Guardiola alisema, “Tuko mweyi Desemba – kama ukiniuliza endapo Liverpool wanaweza kutwaa taji la ligi kuu, nitasema ndio. Kama ukiniuliza sasa hivi kwenye nafasi, Tottenham au Chelsea au Arsenal wanaweza kutwaa taji, nitasema ndio. Kila mtu anaweza kushinda taji la ligi kuu.”
Manchester City itacheza mchezo wake wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Hoffenheim siku ya Jumatano. City tayari wameshafuzu hatua ya mtoano. Baada ya kuikabili Hoffenheim, City ´wataikabili Everton siku ya Jumamosi.
Kauli ya Guardiola kuhusu mbio za ubingwa EPL baada ya kuchapwa 2-0 na Chelsea
Reviewed by Zero Degree
on
12/09/2018 09:05:00 AM
Rating: