Mhasi ateuliwa kuwa Askofu Jimbo la Tunduru
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima imeeleza kuwa, kabla ya uteuzi huo Padri Mhasi alikuwa Paroko katika Jimbo la Mahenge mkoani Morogoro.
“Mwaka 2014 mpaka sasa alikabidhiwa majukumu ya uparoko katika kanisa kuu la Jimbo la Mahenge,” imesema taarifa hiyo.
Mhasi alizaliwa Novemba 30, 1970 na kwa vipindi tofauti amekuwa akitoa huduma mbalimbali kwenye kanisa hilo tangu alipokuwa Padri Julai 3, 2001.
Alipata elimu ya falsafa katika seminari kuu ya Kibosho (1993-1995) na elimu ya teolojia katika seminari ya Mtakatifu Paulo, Kipalapala (1995-1998).
Ametoa huduma sehemu mbalimbali ndani ya Jimbo la Mahenge, msaidizi wa Gombera seminari ya Kasita (2003-2004), Gombera wa seminari hiyo (2009-2014).

Reviewed by Zero Degree
on
12/09/2018 10:50:00 AM
Rating: