Loading...

Rais Kenyatta azindua sarafu mpya Kenya


Benki Kuu ya Kenya imetoa sarafu mpya ambazo zimetawaliwa na michoro ya wanyama. Sarafu hizo nne shilingi moja, tano, kumi na 20.

Urithi wa Kenya wa wanyama wa porini unaonekana dhahiri kwenye sarafu hizo ambazo zimetolewa upya kutokana na utashi wa katiba mpya inayotaka kuondolewa kwa sura za viongozi na kuweka vivutio vya nchi.

Wanyama walio katika sarafu hizo ni tembo, vifaru, twiga na simba ambazo zinaonekana upande mmoja kama ilivyo katika noti.


Rais Uhuru Kenyatta alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa sarafu hizo zilizopewa jina la "Kizazi Kipya cha sarafu".
Rais Kenyatta azindua sarafu mpya Kenya Rais Kenyatta azindua sarafu mpya Kenya Reviewed by Zero Degree on 12/11/2018 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.