Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 9 Desemba, 2018
Paul Pogba na Jose Mourinho |
Paris Saint-Germain watakabiliana na jaribio lolote la kumshawishi Eden Hazard aondoke Stamford Bridge kwenye majira ya joto.
Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku , 25 anaona kuwa hana siku nyingi katika timu ya Manchester United baada ya kukatishwa tamaa na Jose Mourinho.
Manchester City wako tayari kuingia kwenye msako wa saini ya winga wa klabu ya Roma raia wa Uturuki, Cengiz Under.
Imeripotiwa kuwa Arsenal watafikiria kuhusu kumruhusu Mesut Ozil aondoke kwa pauni milioni 25 wakati Inter Milan ikionyesha nia ya kumsajili. (Sun)
Tottenham wanawania saini ya mlinzi wa Bristol City raia wa Uingereya U-21 Lloyd Kelly, wakijiunga na Manchester United, Arsenal na Liverpool.
Cardiff wanatafakari kuhusu kumsaini kwa mkopo mshambuliaji wa klabu ya Everton Oumar Niasse.
Mourinho anasema kwamba Manchester United haina nafasi ya kushinda taji la EPL hivi karibuni kama Manchester City na Liverpool wataendelea kusajili.
Straika wa Uingereza Danny Welbeck, 28, ataachiliwa huru na Arsenal wakati mkataba wake utakapokamilika mwisho wa msimu.
Tottenham wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa uholanzi Tonny Vilhena, kwa mujibu wa ripoti za nchini Italia.
Nyota wa Galatasary Ozan Kabak anafuatiliwa na klabu ya Manchester City kuelekea uhamisho unaoweza kugharimu karibu pauni milioni 20. (Mirror)
Manchester United wamefanya mazungumzo na klabu ya Amiens juu ya uhamisho wa chipukizi wa klabu hiyo Noam Emeran. (Daily Mail)
Manchester United wametajiwa bei ya zaidi ya pauni milioni 90 kwa ajili ya Kalidou Koulibaly, beki wa kati wa Napoli ambaye ni mchezaji anayelengwa zaidi na kocha Jose Mourin. (Times)
Manchester City watafanya jaribio la mwisho kumshawishi Brahim Diaz abaki Etihad baada ya kusita kumuuza kwa pauni milioni 8 kwenda Real Madrid.
Elseid Hysaj |
Chelsea wanafanya maandalizi ya kumnasa beki wa kulia wa klabu ya Napoli Elseid Hysaj mwezi Januari.
Daniel Sturridge anakabiliwa na kufungiwa miezi sita kama atakutwa na hati ya kukiuka masharti ya betting. (Sun)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 9 Desemba, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
12/09/2018 11:35:00 AM
Rating: