Loading...

Dili la Kichuya kwenda Misri mbioni kukamilika



Klabu ya soka ya Simba imeweka wazi kuwa ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili la mchezaji wake winga Shiza Kichuya kwenda kwenye klabu ya Pharco ya Misri.

Simba imethibitisha hilo kupitia taarifa yake kwa umma ambapo imeweka wazi kuwa muda wowote kuanzia sasa itamalizana na Pharco.

Pharco inashiriki ligi daraja la pili nchini humo ambayo ni ya pili kwa ngazi ya ubora ukiacha ligi kuu ambayo hujulikana kama ligi daraja la kwanza.

Makao makuu ya Pharco ambayo ilianzishwa mwaka 2010 yapo jijini Alexandria na Mwenyekiti wake ni Ezz Bashar Helmy.

Kichuya anakwenda kuwa mchezaji wa 3 wa Tanzania anayecheza Misri wengine wakiwa ni Himid Mao na Yahya Zayd.
Dili la Kichuya kwenda Misri mbioni kukamilika Dili la Kichuya kwenda Misri mbioni kukamilika Reviewed by Zero Degree on 1/31/2019 06:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.