Harry Kane ashinda tuzo ya mchezaji bora wa kiume Uingereza
Kane aliiongoza Uingereza kufikia nusu fainali ya kwanza kwenye kombe la dunia baada ya miaka 28, na kwa mujibu wa taarifa ya SkySports anakuwa raia wa kwanza wa Uingereza kutwaa kiatu cha dhahabu kwa kupachika mabao sita.
Nahodha huyo wa Uingereza pia alifunga bao la muhimu lililoipeleka Uingereza kwenye fainali za michuano ya UEFA Nations League kwenye majira ya joto na kufanikiwa kupachika mabao 8 katika michezo 12 mwaka 2018.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kane alisema: "Kuchaguliwa kuwa mchezaji bora Uingereza kwa mara ya pili mfululizo ni kitu cha kujivunia sana. Baada ya mwaka wa aina yake, tuzo hii ina maana kubwa sana kama ambavyo imekuwa ni heshima kubwa sana kutambuliwa na watu muhimu sana - mashabiki.
"Hata hivyo, imepatikana kutokana na msaada mkubwa kutoka kwa wachezaji wenzangu wa Uingereza, Gareth Southgate pamoja na benchi lake zima na tulipewa nguvu kubwa na mashabiki wote waliofanikiwa kufika uwanjani na waliobaki nyumbani.
"Hatutaki 2018 iwe kilele cha mafanikio yetu hivyo tunaendeleza juhudi kwenye michuno ya kufuzu Euro 2020 na fainali ya UEFA Nations League 2019."
Harry Kane ashinda tuzo ya mchezaji bora wa kiume Uingereza
Reviewed by Zero Degree
on
1/18/2019 03:05:00 PM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
1/18/2019 03:05:00 PM
Rating:
