Loading...

Muda wa kustaafu soka bado sana - Mourinho


Jose Mourinho anahisi kwamba bado ana ujuzi mkubwa wa kufundisha soka.

Meneja huyo alichukua mapumziko mafupi lakini sasa amerejea kwenye vyombo vya habari kutoa maoni yake machache siku kadhaa zilizopita. Mreno huyo alipoteza kibarua chake Manchester United kufuatia kichapo cha goli 3-1 dhidi ya Liverpool.

Mkufunzi huyo wa zamani wa klabu ya Chelsea na Real Madrid amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa lakini haonyeshi nia ya kujiunga na klabu yoyote msimu huu. Mourinho ameishi katika mazingira ya utata muda wote alipokuwa United na namna yake ya kukabiliana na vikwazo ilizidi kuwa mbaya siku zake za mwishoni.

Uhusiano wa meneja huyo na baadhi ya wachezaji, ikiwa ni pamoja na Paul Pogba haukuwa mzuri na ulitoa taswira ya matokeo yao huku United ikionekana kuwa ya kawaida sana iwapo uwanjani.

Mourinho alisema, “Nataka kuendelea na kazi yangu.

“Mimi bado ni mdogo sana kiumri, niko kwenye tasinia ya soka kwa muda mrefu sana, lakini nitafikisha miaka 56 ndani ya wiki chahce zijazo.

“Mahali ntakapofanyia kazi ndio nyumbani, mimi ni mtu wa soka la hali ya juu na hapo ndipo nitakapokuwa.”

“Kumaliza katika nafasi ya pili nikiwa na Manchester United kwenye Ligi Kuu ya Uingereza naichukulia kama moja ya mafanikio yangu makubwa katika kazi yangu ya ukufunzi, unasema 'mtu huyu ni kichaa, ameshinda mataji 25 na anasema kwamba kumaliza katika nafasi ya pili ni moja ya mafanikio yake makubwa katika soka’.

“Nitaendelea kusema hili kwa sababu watu hawatambui yanayoendelea nyuma ya pazia na wakati mwingine kwa upande wa kutazama kupitia kamera kila mmoja anakuwa na mtazamo wake.

“Na pia sababu ya mimi kukubali kuwa hapa na nitakubali hata wakati ujao, ambapo sitegemi kuanza kibarua siku za hivi karibuni, ni kutaka kujua zaidi kuhusu mfumo wa soka la sasa na kuujua mfumo huo ni pamoja na kuelewa yanayoendelea nyuma ya kamera.”
Muda wa kustaafu soka bado sana - Mourinho Muda wa kustaafu soka bado sana - Mourinho Reviewed by Zero Degree on 1/20/2019 12:11:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.