Nataka kuona mwanangu anatua England - Baba Samatta
BABA mzazi wa mshambuliaji wa KRC Genk, Mbwana Samatta, Mzee Ally Samatta atasimamia mwanaye atue ndani ya Ligi ya England na kuachana na ofa za nchi nyingine ambazo amezipata.
Samatta ambaye ndiye kinara wa mabao katika Ligi ya Ubelgiji amekuwa akihusishwa kutua katika klabu mbalimbali za England sambamba na Uturuki. Ofa ya juzi ni kutoka Cardiff City ambayo Genk waliipiga chini.
Kwa mujibu wa taarifa ya Spoti Xtra, Mzee Samatta amesema; “Ninachotaka kuona ni kwamba Samatta anatua ndani ya nchi ya England na siyo kwingine ambapo wamekuwa wakimtaka wao aende.”
Nataka kuona mwanangu anatua England - Baba Samatta
Reviewed by Zero Degree
on
1/17/2019 02:28:00 PM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
1/17/2019 02:28:00 PM
Rating:
