Sababu Manula kuwaweka benchi wenzake yatajwa
Mlinda mlango huyo aliyesajiliwa na Simba msimu uliopita, alikosa mechi na KMC akadaka Deogratius Munishi 'Dida' na hakumaliza mechi ya Mbeya City aliumia akaingia Ally Salim.
Kocha wa makipa, Mohammed Mwarami amesema, Aishi ataendelea kudaka kwa sababu hajafanya makosa.
"Hata kwenye mataifa wanayojua soka mfano Manchester United kipa anayejulikana ni De Gea, licha ya timu hiyo kuwa maarufu, wengi hawamjui mlinda mlango wa pili, "alisema Mwarami aliyekuwa mlinda mlango wa zamani wa Simba.
Amesema, nafasi ya kipa ni ya kipekee, hivyo huwezi kumchezesha kila mlinda mlango.
"Kipa anatakiwa kukaa langoni akijiamini, sasa ikitokea amepumzishwa anaporudi anacheza kwa hofu akiogopa kuharibu, "alisema Mwarami.
Amesema, hilo ni tatizo ambalo linaweza kusababisha akafungwa zaidi kwa sababu ya kukosa kujiamini.
Simba imefanya mazoezi yao ya mwisho leo Jumatano asubuhi kwenye Uwanja wa Boko Veterani.

Chanzo: Mwananchi
Sababu Manula kuwaweka benchi wenzake yatajwa
Reviewed by Zero Degree
on
1/16/2019 03:05:00 PM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
1/16/2019 03:05:00 PM
Rating: