Loading...

Tanzia: Baba mzazi wa Alikiba afariki dunia


Baba mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba, Mzee Saleh Kiba amefariki Dunia alfajiri ya leo Januari 17, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa ya GPL, Abuu Kiba ambaye ni mdogo wa Ali Kiba amesema mwili wa marehemu bado umehifadhiwa Muhimbili na msiba upo nyumbani kwao Kariakoo na kwamba mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni.

Inaelezwa kuwa, Mzee Kiba ambaye pia ni baba mzazi wa msanii Abdu Kiba na Zabibu Kiba amekua akiugua kwa muda sasa huku akiendelea kutibiwa.
Tanzia: Baba mzazi wa Alikiba afariki dunia Tanzia: Baba mzazi wa Alikiba afariki dunia Reviewed by Zero Degree on 1/17/2019 10:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.