Loading...

Baada ya Bundi, jingine laibuka Bungeni

Spika wa Bunge Job Ndugai
Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Bungara amesema kuwa hakutishiwa na namna wabunge walivyohangaika kutoka ukumbini mara baada ya kutokea kwa kiasharia cha hatari ndani ya Bunge na wabunge wote kutakiwa kutoka nje ya ukumbi ili kupata taarifa rasmi juu ya kitu kilichotokea.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo, sauti hiyo iliyoashiria hatari ilitokea mapema leo wakati vikao hivyo vikiendelea na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Najma Giga ambapo baada ya muda mfupi alilazimika kuhairisha mkutano huo.

Bungara amesema, "mimi sikukimbia ile sauti ila nilitoka nje kwa sababu ilitokea tahadhari, ila mpaka sasa bado hatujapewa taarifa yeyote kuhusu kilichotokea japo tumetakiwa turudi ndani ya Bunge kwa ajili ya kuendelea na kikao."

Mapema wiki iliyopita Spika wa Bunge, Job Ndugai, alishuhudia kutokea kwa ndege aina ya Bundi huyo akiwa ndani ya ukumbi wa Bunge ambapo alisema, "waheshimiwa wabunge, asubuhi tumeanza kumwona Bundi ndani ya jengo hili, lakini kwa Dodoma Bundi wa mchana hana madhara kwa hiyo ni mambo ya kawaida kabisa,".

Chanzo: Eatv
Baada ya Bundi, jingine laibuka Bungeni Baada ya Bundi, jingine laibuka Bungeni Reviewed by Zero Degree on 2/05/2019 03:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.