Loading...

Barcelona ina mpango wa kumsajili kiungo huyu wa Real Madrid


Rais wa klabu ya Barcelona, Josep Maria Bartomeu ameshangaza ulimwengu baada ya kuweka wazi nia ya klabu yake kutaka kumsajili mchezaji kutoka kwa mahasimu wao, Real Madrid.

Inaeleweka kabisa Isco hayuko kwenye mipango ya muda mrefu ya Santiago Solari na hilo limepelekea mahasimu wao kuanza kumfuatilia kiungo huyo kwa karibu zaidi.

Kimtazamo, ni hitaji lenye tija kwa sababu Mhispania huyo 'anafit' kwenye mfumo wa Barcelona. Ana uwezo wa kucheza katikati na winga. Hata hivyo, uhusiano wa kihistoria kati ya vilabu hivyo viwili ndio unaleta shaka.

Isco ana umri wa miaka 26 sasa na bado ana muda mwingi wa kutosha katika tasinia yake. Wakati Madrid ikionyesha kutokuwa na hitaji la kumtumia sasa kumuuza kwa wapinzani wao wakubwa inaweza kuwa pigo kubwa kwao.

Real bado iko nyuma ya Barcelona kwa pointi 8 kwenye msimamo wa La Liga. Bado wanatafuta mchezaji wa kuziba pengo la Cristiano Ronaldo, huku Florentino Perez akimfanya Eden Hazard kuwa chaguo lake la kwanza kwenye majira ya joto baada ya nyota huyo wa Chelsea kudai kuwa ana mpango wa kuondoka Stamford Bridge baada ya msimu huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Goal, Bartomeu alisema, “Kama makocha wetu wakiomba mchezaji na akawa tayari kuondoka Madrid, bila shaka, tungeweza kumsajili. Lakini haijawahi kutokea tangu mimi niwe hapa.”

“Kila mmoja anajaribu kuifanya timu yake kuwa shindani. Kuhusu Isco? Ndio, kwa vile ni Real Madrid, ningweza kuzungumza na Florentino Perez.”
Barcelona ina mpango wa kumsajili kiungo huyu wa Real Madrid Barcelona ina mpango wa kumsajili kiungo huyu wa Real Madrid Reviewed by Zero Degree on 2/07/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.