Loading...

Sijaona beki kama yondani - Tambwe


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe, tangu amekuja Tanzania kucheza soka, hajawahi kumuona beki wa kumzidi Kelvin Yondani.


Tambwe ambaye amecheza Simba kwa mafanikio, alisema ameshakutana na kucheza na mabeki tofauti, kwa misimu zaidi ya mitano aliyocheza Bongo, lakini Yondani anayekipiga naye Yanga anabaki kuwa beki bora zaidi kuwahi kumuona katika soka la nchi hii.

“Wapo mabeki wengi sana ambao wana uwezo mkubwa, lakini kwa binafsi yangu Yondani anabaki kuwa beki bora zaidi kuwahi kupambana naye na kucheza naye kwa kipindi chote nilichocheza mpira wa Tanzania,” alisema Tambwe ambaye bado hafikirii kustaafu na wala hajui kama Yanga itamuongezea mkataba mwishoni mwa msimu huu.
Sijaona beki kama yondani - Tambwe Sijaona beki kama yondani - Tambwe Reviewed by Zero Degree on 2/07/2019 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.