Loading...

Bodaboda wapigwa marufuku kubeba wanafunzi wa kike


Serikali mkoani Shinyanga imepiga marufuku waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kubeba wanafunzi wa kike wa shule za msingi na sekondari.

Marufuku hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Tellack, ndiye aliyetoa tangazo hilo jana Februari 5, 2019 kwenye maadhimisho ya miaka 42 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanawake (UWT) Mkoa wa Shinyanga.

RC Tellack amesema kila dereva wa bodaboda anatakiwa kuacha mara moja kuwabeba wanafunzi hao wa kike, ili serikali ijiridhishe ni chanzo gani kingine ambacho kimekuwa kikisababisha wanafunzi wa kike kubeba mimba wakiwa masomoni.

“Marufuku waendesha pikipiki mkoani hapa kuwabeba wanafunzi katika vyombo vyao, kwa kuwa inaonyesha kuwa ndio chanzo kikubwa cha wanafunzi na watoto wa kike kubeba mimba, tunataka kujua mara baada ya bodaboda kutowabeba wanafunzi chanzo kingine kitakuwa ni nini,” amesema Tellack.

RC Tellack amesema kama bodaboda atabainika au kukutwa akiwa amembeba mwanafunzi, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Kwa upande mwingine, RC Tellack amesema pia wazazi nao wamekuwa wakichangia kuwa na ongezeko la mimba za utotoni kutokana na kutokuwa wakweli kwa watoto wao juu ya kutoa elimu ya uhusiano.

Chanzo: Nipashe
Bodaboda wapigwa marufuku kubeba wanafunzi wa kike Bodaboda wapigwa marufuku kubeba wanafunzi wa kike Reviewed by Zero Degree on 2/06/2019 07:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.