Loading...

Malengo yetu ni kuchukua ubingwa - Zahera


Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema malengo yake ni kuiweka timu kileleni mpaka msimu wa Ligi Kuu Bara 2018/19 unamalizika.

Mpaka sasa Yanga inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama 61 dhidi ya Azam iliyo na 50 huku Simba wakiwa na 48.

Akili ambayo Zahera ameeleza kuja nayo ni kuhakikisha wanashinda mechi za mikoani ambazo wamekuwa wakipata wakati mgumu kuchukua pointi tatu.

Ameongeza kwa kueleza kuwa wachezaji wake wanapaswa pia kuwa na akili ya kucheza ikiwemo kupiga pasi za kuwapoteza wapinzani haswa wanapokamiwa dimbani.

Kocha huyo mwenye maneno mengi, amewataka pia wachezaji wake kutotumia nguvu nyingi uwanjani bali akili, jambo ambalo halitosababisha kuchoka mapema.

"Malengo yetu ni kuchukua ubingwa, nitahakikisha wachezaji wanatumia akili wakiwa uwanjani na si kukimbia hovyo sababu watachoka, tutapambana kushinda mechi zetu zijazo haswa za ugenini" alisema.
Malengo yetu ni kuchukua ubingwa - Zahera Malengo yetu ni kuchukua ubingwa - Zahera Reviewed by Zero Degree on 2/27/2019 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.